Metropolitani Varsonofi akutana na wanafunzi wa SPbDA kutoka Afrika na Kusini-mashariki mwa Asia. - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Metropolitani Varsonofi akutana na wanafunzi wa SPbDA kutoka Afrika na Kusini-mashariki mwa Asia.

Mnamo Januari 23, 2023, Metropolitani Varsonofi wa St. Petersburg na Ladoga alikutana na wanafunzi wa kigeni wa Chuo cha Theolojia cha St.Petersburg katika Ukumbi-wa-Picha wa ofisi ya Dayosisi. Mkutano huo ulihudhuriwa na wadahiliwa  kwa uanafunzi kutoka Nigeria, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Madagaska, Tanzania, Rwanda, Kenya, na pia wanafunzi kutoka Ufilipino na Indonesia.

Askofu Mkuu aliwapongeza wote kwa kuadhimisha siku kuu ya Krismasi na Epifania ya Bwana na, katika kuagana, akawaachilia neno la baraka za kichungaji.

Kikundi cha wanafunzi kiliambatana na mkuu wa Chuo, Askofu Siluan wa Peterhof. Wakati wa mazungumzo walimu wa Chuo hicho walitoa huduma ya ukalimani, nao ni: Kasisi Mkuu Dimitri Sizonenko (Kifaransa) na N. V. Kolesnikova (Kiingereza).

Mnamo Januari 20, kulifanyika mkutano wa wanafunzi wa kigeni wa Chuo cha Theolojia na Padri Yakobo Smuts (Afrika Kusini) katika chumba cha mihadhara cha idara ya misioni ya Dayosisi ya St.Petersburg.

Wakati wa mkutano, Padri Yakobo alisimulia kuhusu mapito, maisha na uzoefu wake katika  kutenda kazi ya umisionari barani Afrika.

Huduma ya Habari ya SPbDA / Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu

- - - - - - -