Historia ya Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Historia ya Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika

Suala la kuwapokea makasisi wa Kanisa la Kiothodoksi la Aleksandria na kuwaweka chini ya uatamizi wa Patriarkia ya Mosko, lilitafakariwa katika mkutano wa Sinodi Takatifu ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi mnamo Septemba 23-24, 2021 (Jarida Na. 61). Mjadala wa suala hili ulifanyika katika kujibu vitendo vya Patriarki wa Aleksandria Teodore.

***

Katika kuhudumu kwake, muda wote wa kabla ya Ubarikio wa upatriarki, Patriarki  wa Aleksandria Teodore  alitamka mara kwa mara, wazi wazi, kwamba anaunga mkono Uothodoksi wa kanuni nchini Ukraina pamoja na Kanisa la Kiothodoksi la Ukraina lenyewe.Sasa, mnamo mwezi Septemba 2018, akiwa katika ziara ya Odessa, ambayo ilifanyika wiki mbili baada ya kuteuliwa kwa “askofu mkuu” wa Kiev, na Patriarkia ya Konstantinopo, Patriarki wa Aleksandria Teodore alihudumiwa na Metropolitani wa Kiev na Ukraina yote Onufri na Maaskofu wa Kanisa la Kiothodoksi la Ukraina. Katika mahubiri yake, Patriarki Teodore alitoa wito kwa waumini kubaki waaminifu kwa Kanisa la Kanuni la Ukraina na kwa Kiongozi wake: “Bakini katika imani ya Kiothodoksi! Ukraina, Katika historia ya Kanisa letu, kumekuwa na vipindi vigumu, lakini katika nchi ya Ukraina, nchi hii ya kiothodoksi, iliyobarikiwa, kuna Kanisa la kanuni, kuna Mwenyeheri wetu, kaka yetu  Onufri, mtu aliyebarikiwa sana na Mungu, mtawa halisi”;

Mahubiri ya Patriarki wa AleksandriaTeodore mnamo tarehe 09/27/2018 katika ibada ya maombi kwa ajili ya umoja wa Uothodoksi nchini Ukraina

“Nitajitahidi, kwa nguvu zangu zote, kumjulisha kila mtu kuhusu hali ilivyo nchini Ukraina. Kanisa la Ukraina lazima libaki katika uhalisia wake wa kanuni. Hakuna haja ya sisi kuliongezea chochote kipya, kwa sababu tayari lina kila kitu, kama Kanisa la Kiothodoksi la Kristo. Itakuwa dhambi kubwa ambayo tutawajibika kwayo mbele za Bwana katika Ujio  wake wa Pili, endapo tutasababisha japo tone moja la damu kumwagika.”Lakini, mnamo Novemba 8, 2019, Patriarki wa Aleksandria Teodore, kwenye Liturgia kule Kairo, alimwadhimisha kiongozi wa kikundi kimoja kati ya vikundi vya Ukraina, vilivyoasi kutoka kwenye Majimbo Makuu huru ya Kanisa, na akatangaza kutambua kile kinachojiita “Kanisa la Kiothodoksi la Ukraina” – jumuiya ya uasi  iliyopokea “tomosi ya autokefalia” kutoka kwenye mikono ya Patriarki wa Konstantinopo Batolomayo.


Mnamo tarehe 08.11.2019, mjini Kairo, kwenye Liturgia katika Lango Kuu, Patriarki wa Aleksandria Teodore alimwadhimisha kiongozi wa kikundi cha waasi wa Ukraina

Mnamo Novemba 30 ya mwaka huo huo, Patriarki Teodore, wakati akiwa  katika ziara ya Fanar, alihudumu na Patriarki Batolomayo, huku “kiongozi” wa jamii ya waasi wa Ukraina akishiriki katika Liturgia, kati ya maaskofu wanaohudumu.Mnamo Desemba 26, 2019, Sinodi Takatifu ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi iliazimia kutoadhimisha jina la Patriarki wa Aleksandria Teodore katika diptiki, na pia kutoendeleza mashirikiano ya maombi na Ekaristi pamoja naye, na hata maaskofu  wa Kanisa la Kiothodoksi la Aleksandria ambao wameunga mkono na wote watakaosaidia kuhalalisha uasi wa Ukraina katika siku zijazo.

Wakati huo huo, Kanisa la Kiothodoksi la Urusi lilianza kupokea maombi mengi, ya kutaka kujiunga na Patriarkia ya Mosko, kutoka kwa makasisi wa Kanisa la Aleksandria, ambao hawakukubaliana na uamuzi wa Patriarki Teodore wa kuwatambua waasi wa Ukraina, na ambao hawakutaka kubaki chini ya omoforia yake. Kanisa la Kiothodoksi la Urusi lilijizuia kutoa majibu chanya, haraka  haraka, kwa maombi hayo kwa matumaini kwamba Patriarki Teodore angebatilisha uamuzi wake, na kwamba maaskofu wa Kanisa la Aleksandria pia wasingeendelea kuunga mkono kuhalalishwa kwa uasi wa Ukraina. Kwa bahati mbaya, hili halikutokea. Mnamo Julai 28, 2021, Mkuu wa Kanisa la Aleksandria alimtuma mwakilishi wake rasmi, Askofu  wa Babeli Teodore, kwenye hafla iliyoandaliwa na waasi kule Kiev, ambako alisoma salamu kwa niaba ya Patriarki wa Aleksandria. Na mnamo Agosti 13, 2021, Patriarki Teodore alitembelea kisiwa cha Imvros (Uturuki) na, wakati wa Liturujia, ambayo iliongozwa na Patriarki wa Konstantinopo Batolomayo, alihudumu pamoja na mkuu wa kile kinachojiita “Kanisa la Kiothodoksi la Ukraina”, na kisha, katika  maongezi ya faragha naye, alimhakikishia mshikamano na msaada wake mkubwa.


Tarehe 08/13/2021, katika kisiwa cha Imvros kule Uturuki, Patriarki wa  Aleksandria Theodore alihudumu Liturgia pamoja na kiongozi wa kikundi  cha waasi.
Picha: Uothodoksi nchini Urusi

Sinodi Takatifu ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi, katika mkutano wake wa Septemba 23-24, 2021 (jarida Na. 61), ilielezea masikitiko yake makubwa kwa hatua ya  “Patriarki wa Aleksandria Teodore kuhudumu katika ibada pamoja na kiongozi wa  jumuiya ya waasi wa nchini Ukraina, ambayo ilikuwa inakoleza tu ukubwa wa  mgawanyiko kati ya Makanisa yetu.” Kwa kuzingatia yaliyo hapo juu, na kwa kuyatambua maombi mengi ya makasisi wa Kanisa la Kiothodoksi la Aleksandria, kwa Mtakatifu Patriarki wa Mosko na Urusi Yote Kirill, ya kutaka kukubaliwa kuwa chini ya uatamizi wa Patriarkia ya Mosko, Sinodi Takatifu ilimwagiza Askofu Mkuu wa Vladikavkaz  na Alan Leonid, baada ya kuyachambua kwa kina, maombi yote yaliyopokelewa, awasilishe mapendekezo kwenye Sinodi Takatifu. Pia Sinodi ilimteua Askofu Mkuu Leonid kuwa Kasisi wa Patriarkia Takatifu ya Mosko na Urusi Yote, na kumpa cheo cha “wa Klin”,  na kumuondoa katika usimamizi wa dayosisi ya Vladikavkaz, huku  ikibakizia cheo cha u Makamu Mwenyekiti wa Jimbo, Idara ya Mahusiano ya Nje ya Kanisa , na Mkuu wa Dekania ya Parokia za Kipatriarki katika Jamhuri ya Armenia.

***

Sinodi Takatifu ilizingatia mapendekezo ya Askofu Mkuu Leonid wa Yerevan na Armenia katika mkutano wake wa tarehe 29 Desemba 2021 (jarida Na. 100). Askofu Mkuu Leonid alikuwa ameyachunguza kwa makini, maombi yote kutoka kwa makasisi wa Patriarkia ya Aleksandria, akawa amefanya mkutano binafsi na viongozi wa jamii – mapadri kutoka nchi mbalimbali za Afrika, wanaotaka kuwa chini ya uatamizi wa Patriarki wa Mosko. Takriban parokia mia moja za Patriarkia  ya Aleksandria, zikiongozwa nama-abbati wao, zimetangaza nia yao ya kujiunga na Kanisa la Kiothodoksi la Urusi.Sinodi Takatifu, huku ikiona kwamba si vema “kuendeleza msimamo wa kutowakubalia makasisi wa Kanisa la Kiothodoksi la Aleksandria ambao waliwasilisha maombi  ya kutaka kuwa chini ya uatamizi wa Patriarkia ya Mosko,” iliamua ” kuwakubali makasisi 102 wa Patriarkia ya Aleksandria kutoka nchi nane za Afrika na kuwaweka chini ya mamlaka ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi.” Sinodi iliunda Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika, ikiwa na dayosisi mbili – ya Afrika Kaskazini na ya Afrika ya Kusini.Mkuu wa Esarkia ya Afrika  aliamuliwa kuwa na cheo cha “wa Klin”. Askofu Mkuu wa Yerevani Metropolitani wa Klin Leonid aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Afrika, kwa maelekezo ya kusimamia Dayosisi ya Afrika Kaskazini na uongozi wa muda wa dayosisi ya Afrika ya Kusini, na kumpumzisha majukumu ya makamu mwenyekiti wa DECR. Sinodi ilimwacha aendelee na uongozi wa muda wa Dayosisi ya Yerevan-Armenia.

Eneo la uwajibikaji wa huduma za kichungaji la Dayosisi ya Afrika Kaskazini linajumuisha nchi zifuatazo: Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Jamhuri ya Sudan, Jamhuri ya Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Dola ya Eritrea, Jamhuri ya Jibuti. , Jamhuri ya Shirikisho la Somalia, Jamhuri ya Shelisheli, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kamerun, Jamhuri ya Chad, Jamhuri ya Shirikisho ya Naijeria, Jamhuri ya Nijeri, Dola ya Libya, Jamhuri ya Tunisia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, Ufalme wa Moroko, Jamhuri ya Kabo Verde, Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania, Jamhuri ya Senegali, Jamhuri ya Gambia, Jamhuri ya Mali, Burkina Faso, Jamhuri ya Ginebisau, Jamhuri ya Gine, Jamhuri ya Sierra Leone, Jamhuri ya Liberia, Jamhuri ya Kodivaa, Jamhuri ya Ghana, Jamhuri ya Togo, Jamhuri ya Benin.Dayosisi hiyo pia inajumuisha parokia za Stavropol za Patriarkia ya Mosko katika Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Jamhuri ya Tunisia na Ufalme wa Moroko. Sinodi iliamua kuwa cheo cha askofu wa dayosisi hiyo kiwe “wa Kairo na Afrika Kaskazini”.

Katika eneo la uwajipikaji wa kichungaji wa Dayosisi ya Afrika ya Kusini zilijumuishwa nchi zifuatazo: Jamhuri ya Afrika Kusini, Ufalme wa Lesoto, Ufalme wa Eswatini, Jamhuri ya Namibia, Jamhuri ya Botswana, Jamhuri ya Zimbabwe, Jamhuri ya Msumbiji, Jamhuri ya Angola, Jamhuri ya Zambia, Jamhuri ya Malawi, Jamhuri ya Madagaska, Jamhuri ya Morisi, Muungano wa Komoro, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jamhuri ya Kenya, Jamhuri ya Uganda, Jamhuri ya Rwanda, Jamhuri ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Gabon, Jamhuri ya Gine ya Ikweta, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Sao Tome na Prinsipe.Dayosisi hiyo pia inajumuisha parokia ya Stavropol ya Patriarkia ya Mosko katika Jamhuri ya Afrika Kusini. Sinodi iliamua kuwa  cheo cha askofu wa dayosisi hiyo kiwe  “wa Johannesburg na Afrika Kusini”.                                           

***

Mnamo Januari 12, 2022, ilichapishwa  arifa ya Sinodi Takatifu ya Patriarkia ya Aleksandria, juu ya kuanzishwa na kuwekwa wakfu kwa Esarkia ya Kipatriarki ya  Afrika, ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi. Hatua ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi iliitwa “uvamizi” wa eneo la kisheria la Kanisa la Kiothodoksi la Aleksandria, na uamuzi wa kuzindua  esarkia ulielezewa katika hali ya upotoshaji, pamoja na ” kutambuliwa na Patriarki wa Aleksandria, kwa autokefalia ya Kanisa la Kiothodoksi la Ukraina.  Kuhusiana na hili, Sinodi Takatifu ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi, mnamo Januari,2022, ilipitisha azimio maalum. Kusema kwamba Kanisa la Kiothodoksi la Urusi, kama kwamba lilipinga kutambuliwa kwa uhuru wa kujiongoza kwa Kanisa la Ukraina, Sinodi ilijibu: “Taarifa ya namna hiyo imesukwa  katika msingi wa uwongo, tena wa makusudi, kwani Kanisa la Kiothodoksi la Ukraina, kama lilivyokuwa hapo awali, ndivyo lilivyo hata leo – kama sehemu huru ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi, na chini ya usimamizi wake.” “Kanisa la Ukraina halijawahi kuomba autokefalia, na wala halijawahi kupatiwa,” Sinodi ilisema, huku ikisisitiza kwamba “kinachoitwa “autokefalia” kilitolewa na Patriarkia  ya Konstantinopo,  tena si kwa Kanisa la kisheria la Kiothodoksi la Ukraina, ambalo ndilo dhehebu kubwa nchini Ukraine, bali kwa kundi la waasi ambao wamejitenga nalo na wanaendeleza uhasama dhidi yake.”

“Ni kutokana na watu hawa, wasiokuwa wamewekwa wakfu halali, na wasio na baraka za ukuhani, pamoja na washirika wao, walio na mawazo mamoja nao – Patriarkia ya Konstantinopo, kinyume na kanuni, iliundwa “autokefalia ya kanisa” , Na ni muundo huu usio na baraka, Mwadhama Patriarki wa Aleksandria Teodore aliingia katika ushirika nao,” Sinodi ilibainisha katika taarifa yake maalum.

Kulitengenezwa “upotoshaji wa eklesiolojia ya Kiothodoksi, ambao unadhihirika katika utekelezaji wa kile kinachoitwa autokefalia ya Ukraina.”

“Kama ilivyo ada, kutambuliwa kwa uasi wa kule Ukraina, na Patriarki Teodore,kulizusha mtafaruku, ikiwa ni pamoja na ndani ya Kanisa la Kiothodoksi la Aleksandria. Wengi wa makasisi wake walijitokeza hadharani kulitetea Kanisa la kanuni la Ukraina, wakionyesha kutokubaliana kabisa na uamuzi, usio sahihi, wa Mkuu wao, na hawakutaka hata  kuendelea  kumtii mtu ambaye amejiingiza katika njia ya mafarakano.

Kwa miaka miwili, Kanisa la Urusi halikujibu maombi ya makasisi wa Kiafrika waliolijia, bali lilisubiri kwa matumaini kwamba huenda Mwadhama Patriarki Teodore angebadili msimamo wake. Lakini, katika muda wote huu, Mkuu huyu  si tu hakujizuia kumwadhimisha mkuu wa moja ya vikundi vya  waasi wa Ukraina katika diptiki za Askofu Mkuu wa Kiothodosi, bali pia aliingia katika ushirika wa Ekaristi pamoja naye na hata “viongozi” wengine wa makundi hayo ya uasi. Sinodi Takatifu ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi ilisadikishwa na matukio haya ya kuhuzunisha  kwamba kuna  ulazima wa kujibu maombi yaliyokuwa yamepokelewa, na pia, kwa hali kama ilivyojitokeza, kuunda Esarkia  ya Kipatriarki barani Afrika,” Sinodi Takatifu ya Kanisa la Urusi ilitamka. Uamuzi huu “kwa namna yoyote ile, haukulenga kuvamia eneo la kisheria la Kanisa la kale la Aleksandria, bali ulijielekeza kwenye dhumuni  moja tu – la kuwalinda wale makasisi wa Kiothodoksi katika Afrika, ambao hawataki kushiriki katika uhalalishaji wa uasi na mgawanyiko wa Kanisa nchini Ukraina.” Sinodi Takatifu ilitoa wito kwa ” Mtukufu Patriarki wa Aleksandria Teodore II , na pia maaskofu wakuu wengine wa Kanisa Takatifu la Aleksandria, kuacha kuunga mkono mpasuko wa Ukraina, na kurejea kwenye kanuni ili kuhifadhi umoja wa Uothodoksi Mtakatifu.”

***

Mnamo Julai 27, 2023, Mtakatifu Patriarki wa Mosko na Urusi Yote Kirill  alihutubia kikao cha Mkutano wa Kilele wa  Pili wa Urusi—Afrika kule St. Petersburg.Katika hotuba yake, Mwadhama Patriarki alibainisha kuwa, licha ya umbali wa kijiografia, watu wa Urusi na wa nchi za Afrika, wana uhusiano mzuri na wa siku nyingi.”Urusi haijawahi kulichukulia bara la Afrika kama eneo la kukusanyia faida au kama eneo la kufanywa koloni, haijawahi kuongea na watu wa Afrika kwa sauti ya jeuri, wala kujiona kwamba yenyewe iko nafasi ya juu katika ubora au kwamba ina nguvu zaidi. Katika nyakati ngumu za kihistoria, mara zote tumejitahidi kuonyesha mshikamano na kusaidiana,” alisema Mkuu wa Kanisa la Kiothodoksi la Urusi. Mtakatifu Patriarki Kirill alizungumza juu ya uwepo wa kihistoria wa Kanisa la Urusi barani Afrika: “Uwepo kwa Kanisa la Kiothodoksi la Urusi barani Afrika siyo kitu kigeni. Parokia za Kirusi zilianza kuonekana barani humo tangu katikati mwa karne ya XIX – mwanzoni mwa karne ya XX. Hivyo basi, makanisa ya Kirusi yalijengwa kule Abissinia mnamo miaka  1889 – 1896. Parokia ya kudumu ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi nchini Misri ilianzishwa mwaka 1914. Baada ya mapinduzi nchini Urusi, na kutokana na kuibuka  kwa wimbi la wakimbizi kutoka nchini  kwetu, parokia zaidi zilianza kufunguliwa barani Afrika: mnamo mwaka 1920 kanisa la Tunisia liliwekwa wakfu, mnamo mwaka 1922 parokia ilianzishwa kule Aljeria, mnamo mwaka 1927 parokia za Kiothodoksi za Urusi zilifunguliwa nchini Moroko. Mnamo mwaka 1998, nilipata fursa ya kuweka wakfu kanisa la kwanza la Urusi katika Jamhuri ya Afrika Kusini.

Nikiwa katika nafasi ya Uenyekiti wa Idara ya Mahusiano ya Nje ya Kanisa la Patriarkia ya Mosko, na kisha kama Patriarki, kati ya mwaka 1917 na 2016 nilitembelea nchi 18 za bara la Afrika: kaskazini, kusini, mashariki, magharibi na  katikati kabisa. Ninauchukulia mkutano wangu na Bw. Nelson Mandela, nyumbani kwake Soweto, mnamo mwezi Novemba, 1990 kuwa ni tukio maalum sana.

Kwa bahati mbaya sana, mnamo mwaka 2019 Mkuu wa Kanisa la Aleksandria, Patriarki Teodore, kwa hakika, akiwa chini ya shinikizo la kutoka nje, aliamua kutambua kikundi cha waasi nchini Ukraina. Hali hii ya kusikitisha, ilisababisha Kanisa la Kiothodoks la Urusi kuunda Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika, mwezi Desemba 2021. Patriarki wa Aleksandria, akisukumwa na maagizo fulani ya nchi za Magharibi, aliamua kutengeneza mgawanyiko katika  Uothodoksi, na akataka kutulazimisha tukubaliana na hatua hiyo.Kwa hiyo tukaamua kuunda Esarkia katika bara la Afrika. Miongoni mwa kundi letu, si tu Warusi wanaoishi barani Afrika, bali pia wapo wakazi wa asili, wanaofuata imani ya Uothodoksi, na hivi leo ni wafuasi wa Kanisa letu.

Katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu uliopita, Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika imefungua zaidi ya parokia 200 katika nchi 25 za Afrika. Mbali na maendeleo ya huduma za liturgia, miradi mingi ya huduma za kibinadamu na elimu imezinduliwa, kipekee – tafsiri ya vitabu katika lugha za wenyeji, na mengine mengi. Kuanzishwa  kwa Esarkia na juhudi katika utendaji- kazi wake , kumeamsha shauku kubwa na mwitikio mzuri kwa Kanisa  la Kiothodoksi la Urusi, kwa upande wa Waafrika.”

“Kwa wengi, kitu cha muhimu ni kwamba sisi ni Kanisa ambalo linahifadhi kwa uangalifu mapokeo ya utume katika mafundisho, Sakramenti na uzoefu wa kiroho – Kanisa ambalo halipotoshi kanuni za maadili, ili tu kuonekana  kwenda na wakati,” Mtukufu Patriarki Kirill alisisitiza.

Tarehe 11 Oktoba, 2023, Sinodi Takatifu ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi ilikuwa na mjadala wa kutathmini hali ya mambo yalivyo katika Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika (jarida Na. 93). Sinodi iliamua, kutokana na ripoti ya Metropolitani wa Klin Leonid, iliyoelekezwa kwa Mtukufu Kirill, ikiainisha sababu zilizomzuia kutekeleza majukumu yake kikamilifu, kama Askofu Mkuu wa Afrika, kumuondoa Metropolitani Leonid kutoka nafasi hii, kwa shukrani kwa juhudi katika kazi alizofanya, na ikamwachia jukumu la uongozi wa muda wa Dayosisi ya Yerevan-Armenia.  Askofu wa Zaraisk Konstantin aliteuliwa kuwa Kaimu Askofu Mkuu wa Afrika.

Mnamo Februari 16, 2024, Sinodi ya Patriaki ya Alexandria iliamua “kumuondoa” kaimu wa Ufunuo wa Patriaki ya Afrika Askofu wa Zaraisk Konstantin. Aidha Sinodi takatifu ya Kanisa la Orthodox la Urusi, katika mkutano wa Machi 12, iliamua kuzingatia uamuzi huu ambao ulionekana sio wa “haki na batili”, na pia ilimthibitisha Askofu Constantine katika nafasi ya “Patriarchal Exarch of Africa” (gazeti nambari 30).

Mnamo Machi 24, 2024, wakati wa Liturujia ya Kiungu katika Kanisa Kuu la Kristo Mwokozi huko Moscow, Mtakatifu Patriaki Kirill alimpandisha cheo Askofu Konstantin wa Zaraisk hadi cheo cha Mkuu wa mji.