Metropolitani wa Klin Leonid: Makasisi wa Esarkia nchini Afrika Kusini washuhudia kuongezeka kwa shauku kwa Uothodoksi kati ya vijana - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Metropolitani wa Klin Leonid: Makasisi wa Esarkia nchini Afrika Kusini washuhudia kuongezeka kwa shauku kwa Uothodoksi kati ya vijana

Katika ukurasa wake wa “telegram”, Askofu Mkuu wa Afrika, Metropolitani wa Klin Leonid, alizungumza juu ya maendeleo ya misioni ya Esarkia ya Kipatriarki nchini Afrika Kusini.

Padri Yakobo Smutsi anaendelea kutekeleza wajibu wake wa utumishi, akilisha kundi linalokua la waumini wa Kanisa la Kiothodoksi la Urusi nchini Afrika Kusini. “Baada ya mafundisho ya katekesti na mashauriano, Ubatizo unafanywa kwa vijana wa Kiafrika ambao wamekuja kwenye Uothodoksi baada ya safari ndefu ya kuutafuta ukweli,  kutoka kwenye  upinga-dini na kutoka kwenye madhehebu –haribifu, hadi sasa kuifikia imani sahihi na ya kweli,” Askofu alisema.

Askofu wa Kanisa la Kiothodoksi la Urusi alisema: “Shukrani kwa kazi nzuri  ya mtumishi wetu mwingine kule Afrika Kusini, Padri Yohana Rossou, ambaye alitafsiri Liturgia Takatifu pamoja  na maelekezo kwa ajili ya padri, kutoka lugha ya Kiingereza (toleo la Kiingereza lililotayarishwa na  Idara ya Umisioni ya Sinodi,ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi) kwenda lugha ya Kiafrikana, huduma hiyo inafanywa na makasisi wetu kwa utaratibu na desturi za Kanisa la Urusi,” alibainisha Baba Askofu.

Kwa mujibu wa kauli yake, “makasisi wa Esarkia nchini Afrika Kusini wanafurahi kuona ongezeko la shauku kwa Uothodoksi kati ya watu wa eneo hilo, haswa vijana.”

Padri Yakobo alianzisha vikundi vya majadiliano katika mitandao ya kijamii, ambamo wanafanya mikutano ya mtandaoni na kubadilishana mawazo, na mwishoni mwa mwezi Agosti Padri Yakobo atatoa hotuba juu ya Uothodoksi katika kanisa letu dogo kule  Keptauni, ambapo kazi inaendelea kuibadilisha kuwa hekalu la Kiothodoksi. Pamoja na hayo, idara ya uchapishaji, ya kikanda ,ilimuomba Padri Yakobo liweze kuandaa na kuchapisha mfululizo wa makala kuhusu watakatifu wa Kiothodoksi. Kazi hiyo tayari imekwishaanza.

Mnamo Agosti 10-11, 2023, mapadri wa Esarkia- Kasisi Mkuu Zakaria (van Wiik) na Padri Yohana Rossou watatoa hotuba kwenye mkutano wa “Kiafrikana kama lugha ya kiimani”, na mnamo mwezi Oktoba, kwa msukumo wa uongozi wa Chuo Kikuu. cha Stellenboshi (Afrika Kusini), imepangwa mihadhara ya Padri Yakobo Smutsi,  juu ya Uothodoksi, kwa wanafunzi wa kitivo cha theolojia cha chuo kikuu hicho.

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu