Mtakatifu Patriarki Kirill alimtunuku Metropolitani wa Klin Leonid Nishani ya Mtakatifu Innosenti wa Mosko - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Mtakatifu Patriarki Kirill alimtunuku Metropolitani wa Klin Leonid Nishani ya Mtakatifu Innosenti wa Mosko

Mnamo Julai 18, 2023, kwenye sikukuu ya kupatikana kwa nguvu za uadilifu za Mtakatifu Sergius, Abati wa Radonezh, katika kuhitimisha Liturgia Takatifu, katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Utatu Mtakatifu  la monasteri ya Sergius, katika ukumbi wa wanyofu wa Patriarkia, Mtakatifu Patriarki wa Mosko na Urusi Yote Kirill alitunuku tuzo za Kanisa kwa maaskofu na makasisi wa Kanisa la Kiothodoksi la Urusi.

Miongoni mwa waliotunukiwa ni pamoja na Askofu Mkuu wa Afrika, Metropolitani wa Klin Leonid.

Kwa kutambua huduma yake iliyotukuka, ya kichungaji, na kutokana na kuadhimisha  kumbukumbu ya miaka 55 ya kuzaliwa kwake, Metropolitani Leonid alitunukiwa na Baba Patriarki  nishani daraja la tatu (III) ya Mtakatifu Innosenti, Metropolitani wa Mosko na Kolomna.

Askofu Mkuu wa Esarkia ya Afrika 

Shirikisha katika mitandao ya kijamii: