Kundi la tatu la wanafunzi kutoka Afrika lamaliza masomo ya ukasisi - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Kundi la tatu la wanafunzi kutoka Afrika lamaliza masomo ya ukasisi

Tarehe 6 Septemba, 2023, wanafunzi wa masomo ya ukasisi, kutoka Uganda na Kenya, walifanya mtihani wao wa mwisho na kufaulu.

Baada ya kumaliza mtihani, wahitimu hao walipata nafasi ya kutembelea Kanisa Kuu la Kristo Mwokozi mjini Mosko.

Mnamo Septemba 7, mwenyekiti wa Idara ya Misioni ya Sinodi, Askofu Yutimius wa Lukhovitski, aliwatunuku wanafunzi hao vyeti vya kuhitimu kozi hiyo na akawabariki kila mmoja kwa ikoni ya Mpakwa-mafuta Mwana-Mfalme Vladimir Mkuu, aliyewekwa wakfu mahali pa ubatizo kule Chesonesi.

Baba Askofu pia aliwapa wahitimu hao manemane takatifu yenye baraka za  Askofu Mkuu wa Afrika Metropolitani wa Klin Leonid.

Mafunzo hayo  huandaliwa kwa ushirikiano kati ya Idara ya Misioni ya Sinodi na Esarkia  ya Kipatriarki ya Afrika.

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu

- -