Katika Wiki ya 10 ya Pentekoste, Metropolitani wa Klin Leonid aliadhimisha Liturgia Takatifu katika kanisa la Watakatifu Wote kule Kulishki - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Katika Wiki ya 10 ya Pentekoste, Metropolitani wa Klin Leonid aliadhimisha Liturgia Takatifu katika kanisa la Watakatifu Wote kule Kulishki

Mnamo Agosti 13, 2023, Wiki ya 10 baada ya Pentekoste, siku ya kumbukumbu ya Shahidi Mtakatifu Benjamin, Metropolitani wa Petrograd na Gdov, Askofu Mkuu wa Afrika Metropolitani wa Klin Leonid, aliadhimisha Liturgia Takatifu katika kanisa la Watakatifu Wote kule Kulishki jijini Mosko.

Katika huduma hiyo, Mwadhama Askofu Mkuu alisaidiwa na: mkuu wa kanisa la Ufufuo wa Kristo mjini Rabat (Falme ya Moroko) Kasisi Mkuu Maksim Massalitin, makasisi wa kanisa la Watakatifu Wote: mapadri Aleksanda Romanyuk, Dimitri Zakharov, Georgi Maksimov na Shemasi Dionisius Oshuyev.

Wakati wa ibada takatifu, Metropolitani Leonid alimwekea mikono kasisi wa Esarkia ya Kipatriarki nchini Uganda – shemasi Simeoni Odeke kuwa kasisi, na Joji Okello kutoka Kenya – kuwa shemasi.

Mahubiri kabla ya komunio yalitolewa na padri Aleksanda Romanyuk.

Katika kuhitimisha Liturgia, Baba Askofu aliwashukuru waumini waliokuwa wamekusanyika, kwa kushiriki sala ya pamoja, na akawaaga kwa neno la kichungaji.

Askofu Mkuu wa Esarkia ya Afrika

Picha: Ivan Kharlamov

 

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu

-