Vitabu vya maombi, katika lugha ya Kimalagasi, vyachapishwa - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Vitabu vya maombi, katika lugha ya Kimalagasi, vyachapishwa

Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika inaendelea kufanya kazi ya kutafsiri fasihi ya kidini katika lugha za Kiafrika.

Kitabu cha maombi, cha Kiothodoksi, kimechapishwa katika lugha ya Kimalagasi (Madagaska), ambapo kasisi wa Esarkia ya Afrika, Padri Makarii Ratudzunantenaina, alifanya kazi kiyo ya kutafsiri.

Hapo awali vimechapishwa vitabu vya maombi katika lugha za Tiv (Nigeria), Kirundi (Burundi) na pia Kiswahili.

Padri Makarii na Padri Aleksii Erizo, ambao waliwekewa mikono Aprili 2023 na kukamilisha mazoezi yao ya kiliturgia kule Mosko, tayari wamekwisharejea kwao Madagaska. Sasa wanasmbaza vitabu hivyo vya maombi, sanamu takatifu pamoja na misalaba, vyote vikiwa vimeletwa kutoka Urusi kwa ajili ya waumini.

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu

- -