Monasteri ya kwanza, ya wanawake, ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi, inatarajiwa kufunguliwa nchini Kenya - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Monasteri ya kwanza, ya wanawake, ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi, inatarajiwa kufunguliwa nchini Kenya

Askofu Mkuu wa Afrika, Metropolitani wa Klin Leonid, alisema kuwa mtawa Matrona (Dzhepchirchir), baada ya kukamilisha mazoezi ya utawa kule Mosko, ataweza kuwa abbessi na kuongoza nyumba ya watawa nchini Kenya, katika siku zijazo hivi karibuni.

Binti wa kiongozi wa dini katika Wilaya ya Nandi (Kenya), Padri Tito Kipnjena Abigail Jepchirchir, katika utawa, Matrona, kwa heshima ya mbarikiwa Matrona wa Mosko, amekuwa mtawa wa kwanza katika Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika. Aliweka nadhiri mnamo Januari 4, 2023 katika Monasteri ya Mama – wa- Mungu” iliyoko jijini Mosko.

“Yeye bado si abbessi, ila tunatumai kwamba … katika siku zijazo hivi karibuni, Mungu akipenda, baada ya kufanya mazoezi katika Monasteri ya “Mama wa Mungu”kule Mosko, atakwenda Kenya na kuwa  abbessi wetu wa kwanza, wa Kanisa la Urusi. Abbessi-mweusi, ndivyo itakavyosikika,”alisema Metropolitani, katika taarifa yake iliyorushwa na”Solovyov.Live”.

Alibainisha kuwa monasteri itafunguliwa nchini Kenya, ambako watawa watakwenda na kufanya makao.

“Ni wazi kwamba, Wagiriki walizuia, kwa nguvu zote, maisha ya kitawa katika bara la Afrika. Ilai tunafahamu  kwamba jiwe la pembeni la msingi wa kanisa lolote, ni utawa. Mahali ambapo kuna monasteri, maisha ya kiroho hayawezi kuharibiwa,” alihitimisha.

RIA Novosti

 

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu

-