Askofu Mkuu wa Esarkia ya Afrika Konstantin wa Zaraisk - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Askofu Mkuu wa Esarkia ya Afrika Konstantin wa Zaraisk

Alizaliwa tarehe 3 Agosti, 1977 mjini Mosko, katika familia ya kasisi.

Mnamo mwaka1994, alihitimu shule ya sekondari na pia shule ya muziki ya Kanisa katika Hekalu la Upaisho la Krasnogorsk, katika mkoa wa Mosko. Mnamo miaka ya 1990-1995, alihudumu katika nafasi mbalimbali za Hekalu la Upaisho la Krasnogorsk.

Katika miaka ya 1995-1999 alisoma katika Seminari ya Theolojia ya Mosko, na katika miaka ya 1999-2003 – katika Chuo Kikuu cha Theolojia cha Mosko.

Mnamo miaka ya 1997-2002 alikuwa Shemasi-msaidizi wa Metropolitani wa Krutitski na Kolomna Juvenali.

Tarehe 9 Oktoba, 1998, aliteuliwa na mkuu wa Shule za Theolojia za Mosko- Askofu Mkuu Evgeni Vereiski, kuwa Msomaji.

Tarehe 6 Januari, 2001, alibarikiwa na Metropolitani wa Krutitski Juvenali kuwa mtawa, na akapewa jina la Konstantin, kwa heshima ya Shahidi Mtakatifu Konstantin Bogorodski.

Tarehe 15Februari, 2001, aliwekewa mikono na Metropolitani wa Krutitski Juvenali kuwa shemasi, na mnamo Desemba 2, 2002, akasimikwa kuwa kasisi na kuvikwa kitambaa kiunoni.

Mnamo mwaka 2002, aliteuliwa kuwa Makamu wa Mkuu wa Seminari ya Kitheolojia ya Kolomna, katika kazi za ualimu. Tangu 2003 aliongoza kwaya ya Seminari ya Kitheolojia ya Kolomna, pamoja na kufundisha theolojia- linganishi; tangu 2007 – uimbaji wa kikanisa.

Mnamo miaka ya 2003-2006, alikuwa mjumbe wa Baraza la Maaskofu la Dayosisi ya Jimbo la Mosko.

Mnamo mwaka 2004, aliteuliwa kuwa kasisi wa Hekalu la Vvedenski la Seminari ya Kitheolojia ya Kolomna na katibu wa tume ya liturgia ya Jimbo Kuu la Mosko. Mnamo 2005, aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Idara ya Elimu ya Dini na Katekesi ya Jimbo Kuu la Mosko na mjumbe wa Baraza la kuratibu ushirikiano kati ya Wizara ya Elimu ya Mkoa wa Mosko na Jimbo Kuu la Mosko.

Mnamo 2009 aliteuliwa kuwa kaimu-kiongozi wa kwaya ya makasisi wa Dayosisi ya Mkoa wa Mosko, na mwaka 2011 – mkuu wa mafunzo ya umisionari na katekesi wa Dayosisi ya mkoa wa Mosko.

Kwa azimio la Sinodi Takatifu la Julai 26, 2012 (Jarida Na. 67), alichaguliwa kuwa Askofu wa Zaraisk, kasisi wa Jimbo – kuu la Mosko, na akateuliwa kuwa mkuu wa Seminari ya Kitheolojia ya Kolomna.

Mnamo Julai 29, 2012, alipandishwa ngazi na Metropolitani wa Krutitski na Kolomna Juvenali, kuwa Kasisi Mkuu.

Aliteuliwa kuwa askofu tarehe 31 Julai, 2012, katika kanisa la Msalaba kwa heshima ya Ikoni ya Vladimir ya Mama wa Mungu, la Makazi ya Patriarkia katika Barabara ya Chisti mjini Mosko. Aliwekwa wakfu tarehe 12 Agosti katika Liturgia iliyoendeshwa katika kanisa la wakfu kwa Watakatifu Watatu la Seminari ya Kitheolojia ya Kolomna. Ibada takatifu hiyo iliongozwa na Mtakatifu Patriarki wa Mosko na Urusi Yote Kirill.

Tarehe 2 Juni, 2014, katika Chuo cha Theolojia cha Mosko, alitetea tasnifu yake ya shahada ya juu kuhusu mada ya “Historia na mafundisho ya “Kanisa la Agano la Mwisho” (dhehebu la Vissarioni).” Kutokana na ufaulu wa tasnifu yake, alitunukiwa shahada ya “PhD” ya Theolojia.

Kwa azimio la Sinodi Takatifu, la Agosti 25, 2020 (Jarida Na. 67), aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Tume ya Uwepo wa Mahusiano kati ya Makanisa katika Ibada na Taaluma za Kikanisa.

Kwa azimio la Sinodi Takatifu la Aprili 13, 2021 (Jarida Na. 4), aliteuliwa kuwa naibu wa Metropolitani wa Krutitski na Kolomna.

Tarehe 1 Julai, 2022, alichaguliwa kuwa mjumbe wa heshima wa Chuo cha Theolojia cha Mosko.

Kwa azimio la Sinodi Takatifu la tarehe 25 Agosti, 2022 (Jarida Na. 70), iliteuliwa kuwa naibu wa Mtakatifu Patriarki wa Mosko na Urusi Yote, na kuondolewa wadhifa wa ukuu wa Seminari ya Kitheolojia ya Kolomna; ikakabidhiwa jukumu la kuongoza idara ya misioni ya dayosisi ya Mosko (mjini).

Kwa agizo la Mtakatifu Patriarki Kirill, la tarehe 14 Septemba 2022, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Hekalu la Mtakatifu Filipo, la Metropolitani wa Mosko, katika Wilaya ya Meshan.

Tangu Agosti 24, 2023 – Mjumbe wa Tume ya Liturgia ya Sinodi.

Kwa azimio la Sinodi Takatifu la tarehe 11 Oktoba,2023 (Jarida Na. 93), aliteuliwa kuwa Kaimu Askofu Mkuu wa Afrika.

Mnamo Februari 16, 2024, Sinodi ya Patriaki ya Alexandria iliamua “kumuondoa” kaimu wa Ufunuo wa Patriaki ya Afrika Askofu wa Zaraisk Konstantin. Aidha Sinodi takatifu ya Kanisa la Orthodox la Urusi, katika mkutano wa Machi 12, iliamua kuzingatia uamuzi huu ambao ulionekana sio wa “haki na batili”, na pia ilimthibitisha Askofu Constantine katika nafasi ya “Patriarchal Exarch of Africa” (gazeti nambari 30).

Mnamo Machi 24, 2024, wakati wa Liturujia ya Kiungu katika Kanisa Kuu la Kristo Mwokozi huko Moscow, Mtakatifu Patriaki Kirill alimpandisha cheo Askofu Konstantin wa Zaraisk hadi cheo cha Mkuu wa mji.