Kwa mara ya kwanza katika historia ya Esarkia ya Afrika, Metropolitani Leonid alifanya upadrisho wa kikasisi na wa kishemasi - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Esarkia ya Afrika, Metropolitani Leonid alifanya upadrisho wa kikasisi na wa kishemasi

Mnamo Desemba 18, 2022, Wiki ya 27 baada ya Pentekoste, siku ya kumbukumbu ya Mtakatifu Savva, Metropolitani wa Klin Leonid, Askofu Mkuu wa Afrika, aliadhimisha Liturgia Takatifu katika Kanisa la Ufufuo wa Bwana kule Rabat. (Moroko).

Wakati wa ibada takatifu, Shemasi Herman Edianga kutoka Uganda aliwekewa mikono kuwa Kasisi, na Sergius Voemava kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati akawekewa mikono kuwa Shemasi.

Metropolitani Leonid pia alitia saini antiminsi kwa ajili ya parokia za nchi kadhaa za bara la Afrika.

Katika kuhitimisha ibada, kulifanyika tamasha ambalo lilifanywa na  wanafunzi wa shule ya Jumapili, na Askofu Mkuu akakutana na waumini na pia raia wa Urusi walioko huko.

Baadaye Metropolitani Leonid alitembelea Ubalozi wa Urusi, ambako alizungumza juu ya majukumu ya Esarkia ya Kipatriarki na akajibu maswali kutoka kwa wafanyakazi wa uwakilishi huo wa kidiplomasia.

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu

- - -