Ziara ya kikundi cha wamisionari chini ya uongozi wa Padri Georgi Maksimov inaendelea - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Ziara ya kikundi cha wamisionari chini ya uongozi wa Padri Georgi Maksimov inaendelea

Ziara ya kikundi cha wamisionari, chini ya uongozi wa mwenyekiti wa Idara ya Misioni ya Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika- Padri Georgi Maksimov, inaendelea.

Kule Kigali, mji mkuu wa Rwanda, Padri Georgi na mmisionari A.V. Lyulka walikutana na jamii ya Esarkia, ikiongozwa na Msomaji Stefan. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na mkuu wa wilaya.

Kisha kikundi kilielekea mashariki mwa nchi, ambako kilitembelea parokia ya Mtakatifu Serafim wa Sarov kule Churazo, inayoongozwa na Padri Timoteo Renzaho, na parokia ya Mtakatifu Basil Mkuu kule Gator, inayoongozwa na Padri Maksim Mberabahizi.

Padri Georgi Maksimov na A.V. Lyulka waliendesha majadiliano kuhusu misingi ya imani ya Kiothodoksi na jinsi inavyoweza kuelezewa kwa watu wasio Waothodoksi. Kwa kuwa parokia hizi hapo awali zilikuwa katika mazingira ya Kiprotestanti, tahadhari ililazimika kuchukuliwa katika kuzingatia tofauti kuu iliyoko kati ya Uothodoksi na Uprotestanti. Katika hali ya udugu, ya kuaminiana, walijadili njia za kutatua changamoto zinazolikabili Kanisa nchini Rwanda.

Waumini walifurahia sana mikutano hiyo. Kama ilivyobainika, wawakilishi wa Kanisa la Aleksandria walikuwa wanawashawishi waumini wetu ati kwamba Kanisa la Kiothodoksi la Urusi halikuwa limewapokea. Ziara ya watumishi wa Esarkia ikawa ni mhimili wa kukanusha uvumi huo. Mafundisho ya Katekisimu, ambayo kukosekana kwake kumeitesa sana jamii, yataendelezwa na mmisionari A.V. Lyulka. Kwa sasa kazi ya kutafsiri maandiko ya Kiothodoksi kwa lugha ya Kinyarwanda inaendelea.

Askofu Mkuu wa Esarkia ya Afrika

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu