Makubaliano ya ushirikiano kati ya Esarkia ya Kipatriarki, Kamishna wa Haki za Watoto na Mfuko wa Hisani wa “Nchi kwa ajili ya Watoto”, yasainiwa - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Makubaliano ya ushirikiano kati ya Esarkia ya Kipatriarki, Kamishna wa Haki za Watoto na Mfuko wa Hisani wa “Nchi kwa ajili ya Watoto”, yasainiwa

Mnamo Julai 27, 2023, makubaliano ya pande tatu juu ya ushirikiano kati ya Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika, Kamishna wa Haki za Watoto – katika ofisi ya Rais wa Shirikisho la Urusi na Mfuko wa Hisani wa “Nchi kwa ajili ya Watoto” yalisainiwa kule St. Petersburg chini ya mwavuli wa Mkutano wa kilele wa pili wa Urusi – Afrika.

Hati hiyo ilisainiwa na Askofu Mkuu wa Afrika, Metropolitani wa Klin Leonid, Kamishna wa Haki za Watoto- katika ofisi ya Rais wa Shirikisho la Urusi- Maria Lvova-Belova na Mkuu wa Mfuko wa Hisani Aleksei Petrov.

Kwa mujibu wa M. Lvova-Belova, Urusi inapanga kufungua shule katika parokia za Kanisa la Kiothodoksi la Urusi barani Afrika, pia vituo vya watoto yatima na vya misada ya kibinadamu.

Kipekee, kutaanzishwa maabara ya matibabu ya watoto, shamba la kilimo, na mradi wa ufugaji wa kuku.

Makubaliano hayo yatawezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya huduma za kibinadamu na pia kusaidia watoto katika parokia za Kanisa la Kiothodoksi la Urusi barani Afrika. Sasa, kwa mujibu wa Ombudsman wa Watoto, swala lililopo ni kutumia parokia zilizopo.

Kama ilivyoonyeshwa katika ujumbe kwenye ukurasa wa Mfuko”Nchi kwa ajili ya Watoto” kwenye mtandao wa kijamii “VKontakte”, katika makubaliano hayo ” utatekelezwa mradi wa kufunga kiangulio katika kijiji cha Matara, Kenya, chenye uwezo wa kutotoa vifaranga 500 ili kuwezesha ufugaji wa kuku katika parokia za Kanisa la Kiothodoksi la Urusi. Kiangulio hicho kitawezesha kuwa na chanzo cha uhakika cha kuku na mayai kwa ajili ya familia za wanaparokia wenye watoto na zenye kipato cha chini.”

“Pia utatekelezwa mradi wa kuanzisha shamba la kustawisha mazao, ambayo mavuno yake yataelekezwa kwenye familia za waumini wa Kanisa la Kiothodoksi la Urusi zenye uhitaji”, ujumbe unaeleza.

Askofu Mkuu wa Esarkia ya Afrika

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu

-