Mnamo tarehe 23 Februari, 2023, katika parokia ya Mtakatifu Yohana Zlatoust mjini Nyamata (Rwanda), watu 20 walipata Ubatizo Mtakatifu, watu 5 waliingizwa Uothodoksi kwa njia ya Upakwa-mafuta.
Sakramenti hizo ziliendeshwa na Mwenyekiti wa Idara ya Misioni ya Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika, Padri Georgi Maksimov, makasisi wa Esarkia nchini Rwanda – Padri Petro Bikamumpaka na Padri Dimitri Nkundabagenzi.
Watu 25 ni sehemu ndogo tu ya kundi la watu ambao hivi sasa wanapitia uthibitisho, wakijiandaa kuwa wafuasi wa Kanisa la Kiothodoksi la Urusi.
Baadaye, Padri Georgi Maksimov alikutana na Balozi wa Urusi nchini Rwanda, K.D. Chalyan. Pande mbili hizo zilijadili masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano, ikiwa ni pamoja na kuhusika katika maandalizi ya Mkutano wa kilele wa Urusi-Afrika unaotarajiwa kufanyika mwezi Julai mwaka huu.