Kambi ya vijana yaanzishwa kwa ajili ya watoto wa waumini wa Esarkia ya Kipatriarki katika Jamhuri ya Afrika ya Kati - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Kambi ya vijana yaanzishwa kwa ajili ya watoto wa waumini wa Esarkia ya Kipatriarki katika Jamhuri ya Afrika ya Kati

Wiki iliyopita, waumini vijana wa Kanisa la Mtakatifu Andrea mjini Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, walikwenda kwenye kambi ya vijana ya majira ya kiangazi.

Kambi ya watoto wa waumini wa Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika imeanzishwa katika parokia ya Mtakatifu Nikolai Mtendamiujiza, kule Boali.

Katika safari hiyo, watoto wameambatana na padri Sergii Voemava. Wakati wakiwa kambini, Baba padri Sergii anaendesha mafundisho juu ya imani ya Kiothodoksi, anafanya matembezi ya kitalii na kuandaa mashindano na michezo mbali mbali ya burudani.

Tarehe 5 Agosti 2023, katika parokia ya Mtakatifu Nikolai Mtendamiujiza, kule Boali, Padri Sergii aliadhimisha Liturgia Takatifu.

 

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu

-