Mkutano wafanyika kujadili swala la utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa nchi za Afrika - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Mkutano wafanyika kujadili swala la utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa nchi za Afrika

Mnamo tarehe 1 Agosti 2023, katika Kituo cha Jumuiya ya Kiothodoksi ya Wapalestina (IPPO) jijini Mosko, chini ya uenyekiti wa Sergei Stepashin, kulifanyika mkutano kuhusu utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa nchi za Afrika.

Mada hii ilikuwa muhimu sana katika vikao vya Kongamano la Uchumi na Huduma za Kibinadamu la Urusi-Afrika, lililofanyika hivi karibuni kule St.Petersburg.

Kufuatia mkutano huo, Rais wa Urusi Vladimir Putin alitamka kwamba Urusi iko tayari kupeleka nafaka kwa nchi za bara la Afrika zilizo na uhitaji mkubwa, bila kudai malipo yoyote, na kwamba huu ni msaada.

Oleg Ozerov, Balozi Mwandamizi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, mjumbe wa Baraza la IPPO na mkuu wa Idara ya Kimataifa ya IPPO, ambaye alishiriki katika mkutano huo, alifafanua kwa undani juu ya mpango huu wa Rais, na akaelezea uzoefu wa ushiriki wa nchi yetu katika vitendo vya utoaji-huduma za kibinadamu.

Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Afrika, Metropolitani wa Klin Leonid, mjumbe wa IPPO, ambaye pia alishiriki katika mkutano huo, alielezea uzoefu wake katika kutekeleza programu kama hizo, moja kwa moja, katika nchi za Kiafrika, ambapo misaada ya kibinadamu inasambazwa kwa wahitaji kupitia parokia za Kanisa la Kiothodoksi la Urusi.

Katibu Mkuu wa Baraza la Watu wa Yurasia Andrei Belyaninov pia alichangia hoja juu ya uzoefu wake katika muundo na uendeshaji wa misioni hiyo ya kibinadamu katika muktadha wa sheria za kimataifa.

Katika kuhitimisha mkutano huo, uamuzi ulichukuliwa juu ya kuimarisha ushirikiano kati ya IPPO, Kanisa la Kiothodoksi la Urusi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi na Baraza la Watu wa Yurasia, katika utayarishaji na ushiriki katika miradi inayopangwa.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Naibu Mwenyekiti wa IPPO Joji Verenich na Mkurugenzi Mkuu wa IPPO Daniil Burdiga.

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu