Makasisi wa Kanisa la Urusi huendesha ibada barani Afrika kwa lugha mbalimbali - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Makasisi wa Kanisa la Urusi huendesha ibada barani Afrika kwa lugha mbalimbali

– Afrika, ni mchanganyiko wa kipekee wa makabila, mbari, lugha na mila. Baada ya kufika katika ardhi ya Afrika, Kanisa la Kiothodoksi la Urusi lilibaini kikamilifu kiwango kamili cha ukubwa wa “Bara Jeusi,” Askofu Mkuu wa Afrika Metropolitani wa Klin Leonid aliiambia “RIA Novosti”.

Kwa mujibu wa Baba Askofu, ibada takatifu katika makanisa ya Esarkia huendeshwa kwa lugha mbalimbali; Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili, Kiafrikana na pia lugha za kiasili.

Metropolitani Leonid alisisitiza kwamba Kanisa la Kiothodoksi la Urusi “kila siku linapanuka na kwa upendo linaheshimu mila na tamaduni za watu, alimradi hazipingani na mafundisho na kanuni za Kanisa.”

“Upekee wa kumtukuza Kristo kwa kutangamana na tamaduni pamoja na mila za kikabila, ni tunu ya bara la Afrika, raslimali katika hazina ya Kanisa la Kirusi,” Askofu huyo alisisitiza na kuwapongeza watu wote wa bara hilo katika Siku ya Kimataifa ya Utamaduni wa Afrika ambayo huadhimishwa tarehe 24 Januari.

Shirikisha katika mitandao ya kijamii: