V.V. Putin: Kituo cha Urusi cha Elimu ya Kiroho kufunguliwa nchini Uganda - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

V.V. Putin: Kituo cha Urusi cha Elimu ya Kiroho kufunguliwa nchini Uganda

Uganda ni mmoja wa washirika wakuu wa Urusi barani Afrika, Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema katika mkutano na kiongozi wa nchi hiyo Yoweri Kaguta Museveni kule St. Petersburg . Kwa mujibu wa mkuu huyo  wa serikali ya Urusi, nchi hizo zinaendeleza, si tu ushirikiano wa kiuchumi wa faida kwa pande zote mbili, bali pia mawasiliano katika nyanja za huduma za kibinadamu.

“Kuna mipango ya kufungua Kituo cha Urusi cha Elimu ya kiroho,” Vladimir Putin alisema.

“Tunaendelea kutoa elimu ya taaluma kwa wanafunzi kutoka Uganda – hadi sasa takriban raia elfu 4 wa Uganda wamekwishapata elimu katika vyuo vikuu vya Shirikisho la Urusi,” aliongeza.

Vladimir Putin alikutana na Yoweri Kaguta Museveni wakati wa Mkutano wa Kilele wa Pili wa Urusi-Afrika” uliofanyika kule St. Petersburg mnamo Julai 27-28.

 

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu

-