Pongezi za Metropolitani wa Klin Leonid katika kuadhimisha miaka 90 ya Kanisa la Ufufuo wa Kristo kule Rabat. - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Pongezi za Metropolitani wa Klin Leonid katika kuadhimisha miaka 90 ya Kanisa la Ufufuo wa Kristo kule Rabat.

Kwa Paroko wa Kanisa la Ufufuo wa Kristo mjini Rabat, Kasisi Mkuu Maksim Massalitin, waumini wa kanisa hilo.

Heshima ni yako, Baba mpendwa Maksim, kaka na dada zangu!

Kwa moyo mkunjufu ninakupongeza kwa kuadhimisha miaka 90 ya hekalu kuwekwa wakfu!

Kumbukumbu za kihistoria za Kanisa la Ufufuo wa Kristo katika mji mkuu wa Moroko inaonyesha historia ngumu ya kanisa la Urusi nchi za nje katika karne ya ishirini: msafara wa kusikitisha wa “jeshi la wapiganaji weupe” kutoka Urusi, maisha magumu katika nchi ya kigeni, mchakato mgumu wa kujenga nyumba ya Mungu katika mazingira ya  uhaba wa fedha, kurejeshwa kwake  kwenye mamlaka ya Patriarkia ya Mosko.Ujumbe wa kiroho wa uhamiaji wetu ulijumuisha tafakuri ya sababu za kuanguka kwa ufalme, katika uongofu wa toba kwa imani, katika kuleta ukweli wa Uothodoksi kwa ulimwengu wote. Pamoja na ujenzi wa Kanisa la Ufufuo wa Kristo hapa Rabat, mshumaa wa maisha ya kanisa uliangaza tena karne nyingi baadaye katika pembe hii ya kale ya Afrika Kaskazini.

Kanisa hili lililowekwa wakfu na Metropolitani Evlogiy (Georgievsky), ni kitovu cha kiroho kwa vizazi kadhaa vya Warusi wanaoishi Moroko. Kwa usahihi linaweza kuitwa  “ishara ya umoja wa watu wa Urusi”,kwa  ushahidi wa uaminifu wake usio na shaka kwa Uothodoksi na heshima kwa mila za vizazi vya mababu, Sakramenti za kanisa zinafanywa hapa, sala za afya ya walio hai, kwa mapumziko ya marehemu, kwa amani duniani.

Katika siku hii ya kumbukumbu muhimu, kwa sala, ninakutakia furaha ya kiroho katika Bwana, msaada wa Mungu usioshindwa, katika kutekeleza kazi za maisha ya Kikristo, uthabiti wa imani, nguvu imara, amani na maisha marefu!

Naitia Baraka za Mungu juu yako,

+ Leonid,
METROPOLITANI  WA  KLIN,
ASKOFU  MKUU  WA AFRIKA

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu