Kazi inaendelea katika mojawapo ya maeneo ya kipaumbele zaidi kwa misioni ya Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika – elimu.
Matrona (Jepchirchir), mtawa, alianza kujifunza lugha ya Kirusi yeye mwenyewe, hata kabla ya kuweka nadhiri, nchini Kenya. Kule Urusi, mafunzo yake yaliendelea, ila sasa huku akiwa na mwalimu mtaalam.
Mwalimu kutoka Idara ya Kirusi, kama Lugha ya Kigeni, katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Elimu, A.A. Ibrahim, amekuwa akimfundisha Matushka Matrona kwa miezi mitatu, na anakiri kwamba maendeleo yake yanapita matarajio.
Wanafunzi wanaosoma kozi ya ukasisi pia wanajifunza lugha ya Kirusi. Pamoja na hilo, pia, kwa ajili yao, kulifanyika mihadhara juu ya liturgia, theolojia ya kidogmatiki, historia ya Kanisa na skismolojia.
Katika kanisa la Mtakatifu Nikolas Mtenda-miujiza, lililopo katika eneo la Novaya Sloboda jijini Mosko, katika Idara ya Misioni ya Sinodi, chini ya uongozi wa Kasisi Mkuu Igor Davidov, Padri Sergius Voemava (Jamhuri ya Afrika ya Kati) anafanya mazoezi ya liturgia kwa Kifaransa; wanafunzi wa kozi hizo pia huenenda na utii wa madhabahu.
Makasisi wa Esarkia ya Afrika, wanaozungumza Kiingereza, – Padri Danieli Agbaza (Nigeria), Paulo Atangana (Kameruni) na Shemasi Savva Kajava (Malawi), walikwenda Karelia, ambako makasisi hufanya mazoezi chini ya uongozi wa Padri Stanislav Rasputin, huhudumu katika ibada takatifu, huombea wahitaji.
Kumesainiwa Mkataba kati ya Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika na Chuo Kikuu cha Serikali, cha Ualimu, cha Mosko. Tarehe 15 Machi, 2023, K.D. Gorditsa, anayeshughulika na maswala ya wanafunzi wa kigeni, alikutana na V.V. Kruglov, Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Mosko.
Wadahiliwa wanane kutoka Kenya, Madagaska, Kamerun, Uganda na Burundi walijiandikisha katika chuo kikuu hicho kwa kozi ya Kirusi kama lugha ya kigeni. Baada ya kumaliza masomo yao kwa ufaulu mzuri, wataweza kujiunga na shule za theolojia za Urusi, hususani katika Seminari ya Theolojia ya Nikolo-Ugresh, ambapo wataishi kwa muda wote wa masomo yao katika MPSU.
“Namshukuru Mkuu wa Seminari ya Theolojia ya Nikolo-Ugresh Kasisi-Mtawa Methodius (Zinkovski), na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mosko A.V. Lubkov, kwa msaada wao,” Askofu Mkuu wa Afrika, Metropolitani wa Klin Leonid, aliandika katika ukurasa wake.wa mtandao wa “telegram”.