Mazoezi ya Liturgia ya Makasisi wa Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika yanaendelea - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Mazoezi ya Liturgia ya Makasisi wa Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika yanaendelea

Padri Sergii Voemava na wanafunzi wa kozi ya ufundishaji walishiriki katika huduma takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Nicholas kule Novaya Sloboda jijini Mosko,  kwa Kifaransa.

Padri Danieli Agbaza na Shemasi Savva Kajava waliadhimisha Liturgia ya Karama Zilizowekwa Wakfu kwa padri wa Nyumba ya Watawa wa Stavropol ya Mt. Andrea kule Mosko, Abate Dionisius (Shlenov). Huduma hiyo iliendeshwa kwa Kifaransa na Kiingereza. Aidha, Padri Dionisius alifanya mihadhara juu ya patholojia.

“Tunaendelea kushirikiana na Nyumba ya Watawa ya Msalaba Mtakatifu ya Yerusalemu. Kule, pamoja na mazoezi ya liturgia kwa Kiingereza, Baba Padri.Danieli Agbaza na Shemasi Savva Kajava wanajifunza jinsi ya kuoka prosfora na kumimina mishumaa,” Metropolitani wa Klin Leonid aliandika katika ukurasa wake wa “telegram”.

“Ninamshukuru Abate Dionisius (Shlenov), kasisi wa Nyumba ya Watawa wa Stavropol ya Mt. Andrea, na Abbess wa Nyumba ya Watawa wa kike ya Msalaba Mtakatifu ya Yerusalemu, Abbess Ekaterina (Chainikova), kwa msaada wao kwa utume wa Esarkia,” Askofu Mkuu alisema.

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu