Mafunzo ya kawaida ya makasisi wa Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika yaanza - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Mafunzo ya kawaida ya makasisi wa Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika yaanza

Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika, ikishirikiana na Idara ya Misioni ya Sinodi, imeanza kuendesha mafunzo ya kawaida ya makasisi.

Safari hii, masomo na mazoezi ya liturgia yataendeshwa kwa lugha ya Kifaransa.

“Leo tumekutana na wanafunzi kutoka Jamhuri ya Madagaska: Shemasi Makarius Odilon na Aleksei Erizo,”  Metropolitani wa Klin Leonid alitaarifu katika ukurasa wake wa telegram .“Kwa ujumla, makasisi na watumishi wa kanisa kutoka Aivori Kost, Madagaska na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo watahudhuria mafunzo haya. Masomo yataanza katika wiki ya tatu ya Kwaresma.”

Mazoezi ya liturgia ya makasisi wanaozungumza lugha ya Kiingereza, waliowekewa mikono baada ya mafunzo mnamo Desemba 2022 – Januari 2023, hayatakatizwa.

Mapadri Paulo Emme, Sergei Voemava na Shemasi Savva Kajava wanahudumu katika makanisa ya Mosko hadi mwisho wa Kwaresma. Watashiriki ibada za Wiki Takatifu na Pasaka pamoja na waumini wao.

Askofu Mkuu wa Esarkia ya Afrika

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu