Leonid Metropolitan wa Klin: "Tuna matarajio mazuri sana" - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Leonid Metropolitan wa Klin: “Tuna matarajio mazuri sana”

Katika ukurasa wake ya telegramu, Askofu Mkuu Leonid Metropolitani wa Klin alizungumza juu ya dhamira ya Kanisa la Kiothodoksi ya Urusi barani Afrika:

“Tunapanua wigo wa kijiografia. Kwa sasa, hizi ni nchi 23, zaidi ya viongozi wa dini 200, kuna ongezeko la programu za kijamii, za kibinadamu na za elimu.

Kwa ushirikiano wa karibu na Wizara ya Elimu, Wizara ya Afya, na shirika la “Rossotrudnichestvo”, bila shaka, na Wizara ya Mambo ya Nje, tunatengeneza programu zenye bora kwa ajili ya Afrika, ambazo tayari zimeanza kutekelezwa katika nchi nyingi. Tunawasiliana moja kwa moja na wenzetu na washirika wetu katika maandalizi ya mkutano wa pili wa kilele wa kimataifa wa Urusi-Afrika mwezi Julai, ambao, tunatumai, utahudhuriwa na Patriaki Mtakatifu Kirill wa Moscow na Urusi Yote. Hii itakuwa fursa ya pekee ya kufikisha msimamo wa Kanisa la Kiorthodoksi ya Urusi kwa viongozi wengi, marais wa nchi za Afrika, ambao binafsi watahudhuria kongamano hilo huko St. Petersburg

Na nadhani Patriaki wa Moscow na Urusi yote atafanikiwa sana katika kile ambacho Papa Mtakatifu alishindwa katika ziara yake fupi katika nchi kadhaa za Afrika, kwa sababu kundi lake la Kiafrika linampenda, linamheshimu, na linamshukuru kwa kile anachofanya huko kwa kupitia Esarkia Kipatriarki ya Afrika. Na tunaamini kwamba miradi mingi inatekelezwa kwa sasa.

Kwa upande wa Uganda, Rais wa nchi hiyo anasimamia yeye binafsi mchakato huo huko. Ni mtu wa kihafidhina sana, tunajuana kibinafsi. Kwa sasa, tumetengewa moja ya maeneo makubwa nchini Uganda ambapo kitajengwa kituo cha utawala na kiroho cha Kanisa la Kiorthodoksi ya Urusi, hospitali, shule, na majengo mengine, hii ni kulingana na makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa kati ya Patriaki Mtakatifu Rais wa Uganda. Tunaona matarajio mazuri na maendeleo huko.

Hatuna washindani. Ili kuiweka katika lugha nyepesi, tuliingia kwenye makubaliano ya kisheria baada ya Patriarki wa Alexandria kumuunga mkono Patriarki Bartholomew wa Constantinople, kwetu wakawa skismatiki, na kwa hivyo tunaenda kimya kimya kwenye biashara yetu, urithi wetu.

Mambo mengi yanapaswa kusahihishwa, tunakabiliana na masuala mengi na kuanza kufanya kazi tangu mwanzo, jumuiya nyingi za Kikristo za bandia ambazo zilijinasibu kuwa za Kikristo, zinatuomba tufanye nazo kazi na kuzielimisha nini maana ya mafundisho ya Uorthodoksi. Tunafanya hayo yote, vikundi vya wamishonari vinaenda kwa kubadilishana bila kukoma, vinafanya kazi barani Afrika.

Matarajio yetu ni mazuri sana. Kwa sababu Waafrika waliona urafiki ndani yetu, marafiki waliowaona wakati wa Umoja wa Kisovyeti, baada ya hapo, kwa bahati mbaya, kwa miongo mingi, shughuli za Usovieti na Kanisa la Kiorthodoksi ya Urusi zilikuwa hafifu. Lakini mwishowe tulifikia hitimisho kwamba hatutakabidhi nafasi yetu kwa mtu yeyote tena.

Tutaliendeleza bara la Afrika sisi wenyewe, tutawekeza katika elimu sisi wenyewe.

Sasa tunasomesha vijana, wanafunzi 11 walihitimu mwaka wa masomo huko St.Petersburg, kisha wataenda kwenye kozi kamili ya miaka minne ya elimu ya theolojia. Watoto wanasoma katika Chuo Kikuu cha ualimu cha Moscow. Siku moja tuliadhimisha Siku ya Lugha ya Kirusi ambayo ni siku ya kuzaliwa kwa Pushkin, wanafunzi hao walisoma kikamilifu sala ya “Baba yetu” na mashairi ya Pushkin. Yaani watu wanaanza kupata tamaduni zetu, pia wanaanza kupata habari zetu Njema kuhusu Kristo kutokana na mapokeo, na tunafurahi sana kwamba tuna nafasi hiyo ya kuwahabarisha ndugu zetu, yaani ndugu na marafiki. Ndivyo wanavyotuona, kwa sababu Kanisa la Kiorthodoksi ya Urusi, kama serikali ya Urusi, halijawahi kujihusisha na ukoloni mamboleo katika bara la Afrika”.

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu