Ziara ilianza kwa kufanya mkutano wa kichungaji na makasisi wa kanisa la Esarkia nchini Kameruni. Washiriki walijadili mipango ya maendeleo ya utume nchini humo,wakatatua masuala kadhaa ya kiutawala pamoja na changamoto zinazoikabili parokia.
Tarehe 12 Februari 2023, katika Wiki ya Mwana Mpotevu, siku ya kumbukizi ya walimu wa kiekumeni na watakatifu Basil Mkuu, Gregori Mtheolojia na Yohana Zlatousti, iliadhimishwa Liturgia ya upatanisho katika kanisa la Ufufuo wa Kristo mjini Yaunde – mji mkuu wa Kameruni. Ibada takatifu iliongozwa na Padri Georgi, huku makasisi wa Esarkia wakihudumu pamoja naye.
Katika kuhitimisha la ibada, Padri Georgi alitunuku vyeti vya heshima kwa waumini vijana – washindi wa shindano la Mchoro wa Uothodoksi na akawapa tuzo za ukumbusho.
Siku hiyo hiyo, Baba Padri Georgi alikutana na “askofu” wa kikundi kisicho na uhalali kisheria, akitaka kujiunga na Kanisa la Kiothodoksi la Urusi. Kwa mujibu wa taratibu, kuhamia kwake kunawezekana endapo tu atakuja kama mtu wa kawaida.
Aidha, mara kadhaa kumepokelewa maombi ya makasisi wa Metropolia ya Kameruni ya Kanisa la Aleksandria, wakitaka kuhamia Patriarkia ya Mosko, na yanafikiriwa.