Sinodi Takatifu yatambua azimio la “kushushwa cheo” kwa Metropolitani wa Klin Leonid kuwa halina nguvu ya kikanuni - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Sinodi Takatifu yatambua azimio la “kushushwa cheo” kwa Metropolitani wa Klin Leonid kuwa halina nguvu ya kikanuni

Katika mkutano wa Sinodi Takatifu ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi, uliofanyika Desemba 29 , washiriki walijadili azimio la Sinodi ya Patriarkia  ya Aleksandria  kuhusu  “kushushwa  cheo” kwa Askofu Mkuu wa Afrika, Metropolitani wa Klin Leonid.

JARIDA Na. 136

WATOA  HOJA ; juu ya azimio la Sinodi ya Patriarkia ya Aleksandria  kuhusu “kushushwa  cheo”  kwa  Askofu Mkuu wa Afrika, Metropolitani wa Klin Leonid.

Hoja:

Kuhusiana na kutambuliwa  rasmi kwa kanisa linalojiita Kanisa la Kiothodoksi la Ukraina na Patriaki Theodore wa Aleksandria tarehe 8 Novemba, 2019, na kisha yeye kumuadhimisha  mkuu wa muundo huu usio wa kikanuni,  katika liturgia, Sinodi Takatifu, katika mkutano wake wa tarehe 26 Desemba, 2019  ilithibitisha kutokuwepo tena  kwa uwezekano  wa kuadhimisha jina la Patriarki Theodore wa Aleksandria katika diptiki, na pia kuwa na ushirika naye katika maombi na Ekaristi na ikasitisha mawasiliano ya kikanisa na maaskofu wa Kanisa la Kiothodoksi  la  Aleksandria, ambao “waliunga mkono au katika siku zijazo wataunga mkono uhalalishwaji  wa  uasi na mgawanyiko katika Kanisa la Ukraina” (jarida Na. 151).

Baadaye, Patriarka Theodore wa Aleksandria , si tu hakupinga  kumwadhimisha mkuu wa kikundi  kilichotajwa  hapo  juu, bali pia  alihudumu naye katika liturgia kwenye kisiwa cha Imvros tarehe 13 Agosti, 2021. Akijibu maombi mengi kutoka kwa makasisi wa Patriarkia  ya Aleksandria, ambao hawakutaka  kuwa  washiriki katika matendo ya kuvunja  kanuni , yaliyotekelezwa na Patriarki  wao, na  wakaomba wakubaliwe kuwa chini ya mamlaka ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi, na kwa kuzingatia ukweli kwamba Patriarki Theodore ndiye  aliyefungua  njia ya mgawanyiko  huo, Sinodi Takatifu, katika mkutano wake wa tarehe 29 Desemba, 2021(jarida Na. 100) iliamua kuunda  Esarkia  ya Kipatriarki  ya Afrika)  na  kumteua Metropolitani wa Klin Leonid  kuwa mkuu wake.
Sinodi Takatifu, katika taarifa yake ya Januari 28, 2022, ilibainisha kwamba uamuzi juu ya kuundwa kwa esarkia, "uliopitishwa  huku kukiwa  na mazingira  ya kutambuliwa  kwa waasi wa Ukraina  na Patriarki  wa  Aleksandria, kwa namna yoyote ile kusichukuliwe kuwa ni kauli ya madai  ya kupokonya eneo la kikanuni  la Kanisa la kale la Aleksandria, bali  unaofuata lengo  pekee – la kutoa  ulinzi wa kikanuni  kwa wale makasisi wa  Kiothodoksi  barani  Afrika,  ambao  hawataki kuwa  washiriki katika uhalalishaji   wa uasi na  mgawanyiko nchini Ukraina."
Barua za Patriarki Theodore wa Aleksandria,  za Januari 12 na Februari 14, 2022,  zilizotumwa kwa Patriarki wa Kanisa la Kiothodoksi la Urusi zilikuwa  na  tishio  la "kushushwa  cheo"  kwa Metropolitani wa Klin Leonid.  Patriarki  wa Mosko na Urusi Yote Kirill alituma  jibu  kwa jumbe  mbili (barua  za Januari 18 na Machi 5, 2022). Katika barua yake ya mwisho, Mwadhama Patriarki,  kipekee  alimwambia Patriarki Theodore, "kwamba maamuzi yoyote ya kimahakama ya Kanisa lako kuhusu Metropolitani wa Klin Leonid  au maaskofu wengine au makasisi wa Kanisa letu, yatatambuliwa  nasi  kuwa  hayana nguvu ya kikanuni  na  ni  batili."
Mnamo tarehe 22 Novemba, 2022, Sinodi Takatifu ya Patriarkia  ya Aleksandria ilipitisha azimio  "kuhusu  kushushwa  cheo  kwa Metropolitani wa Klin Leonid."
WAAZIMIA:
Katika kutilia  maanani kuegemea kwa  Patriarki Theodore  wa Patriarkia ya Aleksandria  kwenye  mpasuko  (kutambua kwake uasi wa kikundi cha watu ambao hawana neema ya ukuhani,  na waliotengwa na Kanisa, na kuwa  na ushirika wa Ekaristi nao, kuunga mkono mgawanyiko ndani  ya Kanisa la Kiothodoksi la  Ukraina), na kwa kuzingatia  kanuni, mila  na taratibu zinazotambulika kwa ujumla,  za  kwamba  Kanisa moja linalojitawala lenyewe  halina  mamlaka ya kimahakama dhidi ya  Kanisa lingine ambalo nalo linajitawala lenyewe, azimio  la Sinodi ya Patriarkia  ya Aleksandria  kuhusu  "kushushwa  cheo"  kwa  Askofu Mkuu wa  Afrika, Metropolitani wa Klin Leonid, na maamuzi mengine yote  yanayofanana  na  hayo, kuhusu makasisi wa Kanisa la Kiothodoksi la Urusi, kuwa hayana nguvu ya kikanuni  na  ni batili.
Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu