Mihadhara juu ya Maandiko Matakatifu na Katekisimu yatolewa katika parokia mbili za Esarkia nchini Kenya - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Mihadhara juu ya Maandiko Matakatifu na Katekisimu yatolewa katika parokia mbili za Esarkia nchini Kenya

Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika inaendelea na utekelezaji wa miradi ya uelimishaji katika nchi ilizo na wajibu wa kichungaji kwake.

Mmishonari na mwalimu A.V. Lyulka yuko nchini Kenya, ambako anatoa mafundisho ya Maandiko Matakatifu na Katekisimu.

Mafundisho  hayo yanahudhuriwa na makasisi, makatekista, vijana, wanaharakati  “Orthodox Mother Unions” pamoja na waumini.

Aleksanda Vyacheslavovich anaendesha mafunzo katika parokia mbili, kati ya tisa, za Esarkia nchini Kenya; Parokia ya Kati na ya Meru. Mihadhara hiyo inatafsiriwa kwa Kiswahili. Washiriki wanaitikia kwa shauku na shukrani kwa kupatiwa fursa ya kujifunza zaidi kuhusu Injili, Uothodoksi, kanuni na taratibu za Kanisa la Kiothodoksi la Urusi.

Katika siku za usoni, mihadhara hii ya uelimishaji inapangwa kufanyika katika parokia zote za Kenya.

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu