Herman Ediyangu wa Uganda, aliyewekewa mikono kuwa shemasi katika Patriarkia ya Aleksandria mnamomwaka 2018, alikuwa mmoja wa makasisi wa kwanza wa Kiafrika kutuma maombi ya kuhamia kwenyeKanisa la Kiothodoksi la Urusi kufuatia kutambuliwa kwa mgawanyiko wa Ukraina na Patriarki Theodore II wa Aleksandria. Mnamo tarehe 18 Desemba, 2022, kulifanyika upadirisho wake — Baba Herman akawa Mwafrika wa kwanza kuwekewa mikono kuwa kasisi chini yamamlaka ya Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika. Katika mahojiano RIA Novosti Baba Herman alizungumza juu ya upekee wa Uothodoksi baraniAfrika.
Baba Herman, unajisikiaje kuwa mtu wa kwanza kutoka Afrika kuwekewa mikono ya upadirishokatika Kanisa la Urusi?
– Ninahisi kubarikiwa, ni mnyenyekevu na mwenye furaha sana. Kwangu mimi, hii ni hatua nyingine ya kusonga mbele kwenye ushiriki wa maendeleo ya kiroho ya watu wetu, ili kuokoa roho nyingi zaidi katika siku zijazo. Nimejaa matumaini!
– Esarkia imekuwepo kwa mwaka mzima sasa. Je imeleta mambo gani mapya katika maisha ya parokia za barani Afrika? Ni kwa jinsi gani huduma yako ya liturgia imebadilika?
– Liturgia ya Kirusi ina maelezo zaidi kuliko ya Kigiriki. Ninapotazama huduma ya Kigiriki, naona kwamba baadhi ya vipengele vimeondolewa, kwamba imekuwa fupi. Ya Kirusi ina hatua zote zilizokuwepo katika Liturgia ya tangu mwanzo. Ni ndefu, ina maelezo mengi zaidi.
– Mnahudumu kwa lugha gani?
— Tunatumia lugha zetu za asili. Binafsi, ninahudumu kwa ki-Ateso, lugha inayozungumzwa katika eneo letu la dekania ya Soroti. Lakini kaskazini mwa Uganda, wanahudumu kwa ki-Ocholi, ki-Lango – lugha za asili za watu wa maeneo hayo. Ila wakati mwingine sisi hutumia pia Kiingereza ili kuelewana nao vizuri zaidi;kwa mfano, kama kwenye ibada au huduma kuna waumini ambao hawajui lugha ya asili ya eneo-husika, basi huwa tunahamia kiingereza kwa ajili yao.
– Umehamia Kanisa la Urusi ukitokea Patriarkia ya Aleksandria. Kwa nini uliamua kujiunga nalo? Ulifahamu nini kuhusu Urusi na kuhusu Kanisa la Urusi, kabla ya uhamisho?
– Niliwekewa mikono kuwa shemasi katika Kanisa la Aleksandria mnamo mwaka 2018. Wakati mgawanyiko ulipoanza, na mpasuko huo wa “Kanisa la Kiothodoksila Ukraina” ulipotambuliwa, tuligundua kuwa hili linapingana na kanuni, na kwamba kwa hapa Kanisa la Kiothodoksi la Urusi ndilo pekee linalohifadhi hadhi yake. Baada ya kutambua hili, binafsi niliamua kwamba nitafuata mafundisho ambayo Kanisa hili linatoa, na nikaweka nia ya kujiunga nalo. Sasa nimepata mafundisho pia katika Kanisa la Kiothodoksi la Urusi, nimepokea upadrisho na ninamshukuru Mungu kwa hilo.
– Je, waumini wako, na Waganda kwa ujumla, wanajua nini kuhusu Kanisa la Urusi?
– Watu katika nchi yetu wanajua kwamba Kanisa la Kiothodoksi la Urusi ndilo lililoenea zaidi nchini Urusi, na ambalo limejengwa katika misingi na taratibu za ukuhani, mafundisho na imani, ambazo zimedumishwa tangu nyakati za mitume. Ni muhimu kwamba ufahamu kuhusu hili uenezwe. Watu wengi tunaowahudumia kwa mahubiri wanaliangalia Kanisa la Urusi kwa hisia-chanya na wanaikubali omoforia yake, kwa sababu wanavutiwa na uhafidhina-chanyawake katika kuhifadhi mila, taratibu na mafundisho ya kweli.
– Parokia za Uganda zinaishi vipi? Wana mahitaji gani; vyombo vya usafiri, majengo kwa ajili ya ibada, maji, elimu, au kitu gani kingine?
– Kuwa katika “ulimwengu wa tatu”, Afrika, bila shaka, ina mahitaji mengi. Nitaanza na matatizo yanayowakabili makasisi kama mimi, hasa nchini Uganda. Kikwazo kikubwa kwetu ni ukosefu wa vyombo vya usafiri. Achilia mbali magari , hatuna hata pikipiki. Gari linakuwezesha kusafiri hata katikakipindi cha mvua, na ikiwa unahitaji kuendesha ibada ya mazishi au Liturgia, basi utalazimika kusubiri mvua ikatike kwanza. Kwa Afrika, hili ni tatizo la msingi, na msaada wowote wa usafiri ungetufaa sana.
Wanaparokia – watu tunaowahudumia – pia wanakabiliwa na changamoto nyingi. Mojawapo ni ukosefu wa elimu bora. Ulimwengu hupanga programu za elimu ya kibinadamu, lakini hii, sana sana, huchangia tu ongezeko la ukosefu wa ajira. Kwa maoni yangu, watu wa Afrika sasa wanahitaji kushirikishwa katika kozi za taaluma za ufundi. Kwao hii ni muhimu sana, kwani inawawezesha, mara tu baada ya kumaliza masomo, kufanya kazi katika taalama waliyoipata na kuinua kipato chao. Ninashawishi watu kwenda kusomea ujenzi, ufundi-cherehani, umakanika, ufundi – seremala, hizi zote ni taaluma zinazoheshimika sana.
Tatizo kubwa jingine ni maji na upatikanaji wake. Kuna visima virefu vichache, na katika vijiji vingi kuna vidimbwi tu, ambavyo maji yake si salama kwa kunywa, watu wanaugua sana.
Hakuna vituo vya kutosha vya matibabu ya kiwango-stahiki. Magonjwa yanaenea, na hospitali kwa kawaida ziko mbali sana na vijiji, na hata hivyo, mara nyingi huwa hazina dawa. Kwa mfano, ukigundulika kuwa una malaria, basi utaelekezwa kwenda kwenye maduka-binafsi ya dawa. Kwa hiyo vijiji na parokia zetu zinahitaji huduma za matibabu ya uhakika.
Je, kwa mawazo yako, Kanisa la Urusi, na waumini wenzako wa dini nchini Urusi, wanaweza kusaidia katika kukidhi mahitaji haya? Je, Elimu ya Kirusi na wataalamu wa Kirusi wanaweza kusaidia katika hili?
– Ndiyo, kwa sababu tunapojifunza kutoka kwa watu kutoka nchi zilizoendelea, kama vile Urusi, tunajiendeleza. Ninajua kwamba wamefunzwa vyema na wanaweza kutoa huduma bora. Uganda inawangojana itawapokea kwa mikono miwili, ni nchi yenye hali ya hewa nzuri na watu wakarimu.
Msaada wa waumini kutoka Urusi, bila shaka, pia nimuhimu sana kwetu. Hii inaweza kuwa katika hali ya kutafuta rasilimali na kupanua miradi ya ujenzi wa, kwa mfano, mahospitali – angalau hospitali moja kaskazini, moja kusini na na moja mashariki mwa nchi – hali ya maisha ya watu ingeimarika sana, ikiwa ni pamoja na ya kiroho: mtu mwenye afya njema ana nafasi nzuri ya kujitoa kikamilifu katika kumtukuza Bwana.
– Je, kuna uhusiano gani, hivi sasa, na wanaparokia waliobaki katika Patriarkia ya Aleksandria?
– Katika ngazi ya watu binafsi, ngazi ya chini, uhasamani mdogo sana, karibu hakuna chuki kabisa. Pamoja na yote yaliyojili, hawa bado ni watu wanaoishi katika jumuiya moja, wakishiriki kila kitu pamoja, isipokuwa Liturgia.
– Na je jumuiya za Patriarkia ya Aleksandria ziliitikiaje kujiunga kwa makasisi kwenye Kanisa la Urusi? Je, wewe na waumini wenzako,mmekabiliwa na vitisho, ubaguzi au vurugu zozote kutoka kwao?
– Mwanzoni, Kanisa la Aleksandria lilishikwa na hasirasana kwa wale tuliohamia kanisa la Urusi. Walitunyang’anya mavazi, vifaa vya kiliturgia, hatawatoto wetu waliachishwa shule na hivyo kulazimika kukaa nyumbani. Hali hii iliathiri sana elimu yao kwa sababu wazazi wengi walikuwa wanategemea ufadhili wa kanisa muda wote. Lakini sasa, kwa maoni yangu, Kanisa la Aleksandria linaanza kutambua kwamba,kwa kuhodhi hasira na chuki dhidi yetu, hawatapata ushindi: kwamba katika swala hili, ni sisi tu ndio tutabakia washindi.