Salamu za Pasaka za Patriarki Kirill kwa Makasisi Wakuu, Makasisi, Mashemasi, Watawa na Waumini wote  wa Kanisa la Kiothodoksi  la Urusi - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Salamu za Pasaka za Patriarki Kirill kwa Makasisi Wakuu, Makasisi, Mashemasi, Watawa na Waumini wote  wa Kanisa la Kiothodoksi  la Urusi

Patriarki wa Mosko na Urusi Yote Mtakatifu Kirill alituma salamu za Pasaka kwa makasisii wakuu, makasisi, mashemasi, watawa na waumini wote wa Kanisa la Kiiothodoksi la Urusi.

Wapendwa katika Bwana, Waheshimiwa Maparoko, waheshimiwa Mapadri na Mashemasi, na watawa wapenda-Mungu; kaka na dada zangu!

Kwa Wakristo wa Kiothodoksi mnaoishi katika nchi mbalimbali ulimwenguni kote, mnaokaa makanisani na majumbani mkisali, ninawaelekea ili kukupongezeni, kutoka kwenye kilindi cha moyo uliojaa furaha ya kiroho katika sikukuu kuu ya Pasaka Takatifu na, kwa mujibu wa mila na taratibu  za  enzi na enzi, kutangaza ushindi kwamba:

Kristo Amefufuka!

Kwa milenia mbili sasa, Kanisa Takatifu, kwa maneno haya ya shangwe za ushindi, limekuwa likiwahubiria watu habari njema ya wokovu utokao kwa Mungu. Maneno haya yana moto wa imani yetu, yana nguvu ya upendo, msingi wa tumaini, na ni jiwe kuu la msingi wa Kanisa, lengo la ujumbe wa Agano Jipya kwa ulimwengu, mwanga usiofifia wa uelimishaji na wa msukumo mpya, kiini cha maisha ya Ukristo na mustakabali wetu.

Haijalishi nini kitakachotokea katika ulimwengu ubadilikao, wakati mwingine usio na utulivu na uliovurugwa na mizozo, haijalishi ni magumu na majaribu gani yanatupata, tunajua, tunaamini na tunahubiri: furaha ya Pasaka ya Mwokozi Mfufuka iko imara, haibadiliki na inashinda vyote.

Ni nini maana ya siku kuu hii ya Kikristo? Kwa jina la nani na kwa nini Mwana wa Mungu alishuka duniani, akachukua umbo la mtumwa (Flp. 2, 7), akateswa, akasulubishwa msalabani na akafufuka? Na sisi, watu wa karne ya ishirini, tunapaswa kufanya nini ili kweli tuwe washiriki na warithi wa ushindi alioupata Kristo juu ya kifo?

Kanisa linatupatia majibu ya maswali haya. Linashuhudia kwamba kwa Mwana wa Mungu aliyefanyika mwili kutoka kwa Bikira aliyebarikiwa sana, Adamu alizaliwa, Adamu aliitwa, kiapo kilihitajika, Hawa aliwekwa huru, kifo kikanyamazishwa, na sisi tuko hai (Jumapili ya Theotokos katika sifa, sauti 2). Kwa kweli, Bwana hutuhuisha kwa upendo wake, hutuweka huru kutokana na hofu ya kifo na uharibifu, huponya udhaifu wa akili na wa mwili, hutusaidia katika magumu na majaribu, hutufariji katika huzuni na dhiki, hutusaidia kuifuata njia ya wokovu inayotupeleka kwenye uzima wa milele, pale Mungu atakapofuta kila chozi katika macho ya wanadamu, na kifo hakitakuwapo tena; hakutakuwa na kilio wala ugonjwa tena (Ufu 21:4).

Baada ya kukamilisha kazi ya ukombozi, Bwana, kwa dhabihu yake msalabani na Ufufuo mtukufu, alifungua milango ya paradiso kwa kila mtu. Kuanzia wakati huo hadi sasa, kila mtu

anapewa nafasi ya kumwona Kristo kwa nafsi yake yote kuwa  ni Mungu wa kweli na Mwokozi, ambaye hushusha nguvu iletayo neema kwa ajili ya maisha ya haki na kushiriki kikamilifu katika mabadiliko ya ulimwengu.

Mtakatifu Nicholas wa Serbia, mtheolojia mashuhuri wa karne iliyopita, akitafakari juu ya Pasaka, aliandika hivi: “Kristo amefufuka – kwa hiyo uzima una nguvu zaidi kuliko kifo. Kristo amefufuka – hivyo wema una nguvu zaidi kuliko uovu. Kristo amefufuka – hiyo ina maana kila kitu

matumaini ya wakristo ni halisi. Kristo amefufuka – hivyo shida zote za maisha zimetatuliwa” ( Fikra juu ya mema na mabaya). Na furaha hii ya Pasaka, furaha ya ushirika na Mungu na uthibitisho wa maisha mapya (Warumi 6, 4) juu ya kanuni za wema na haki inazifikia mioyo ya mamilioni ya Wakristo, inawachochea kufanya matendo ya upendo na huruma, inasaidia kushinda dhiki, kutoa faraja katika shida, inawapa matumaini waliokata tamaa, inaimarisha mioyo iliyozimia.

Katika siku kuu nzuri ya Pasaka, sala zetu maalum zinaelekezwa kwa Mungu kwa ajili ya watu walioko katika eneo la vita. Kama Wakristo, hatuwezi kutojali shida na dhili za ndugu na dada zetu, ambao mioyo yao imeunguzwa na moto wa migogoro ya ndani, kwa hiyo tunamtolea Bwana maombi maalum kwamba Yeye, kwa rehema na fadhili zake

, aponye miili na, zaidi ya yote, majeraha ya kiroho, afariji kila huzuni kwa ndugu zetu watu ambao wameibuka kutoka kwenye kisima kimoja cha Ubatizo cha Dniepa, amani ya kudumu na ya kweli.

Kama vile njia ya kidunia ya Mwokozi ilijaa mateso na upendo wa kujitoa-mhanga kwa watu, vivyo hivyo tunaitwa kuwa kama Yeye katika kuwahudumia jirani zetu. Baada ya yote, chochote kile, hata huruma  ndogo  tu, kuushinda ubinafsi wa mtu mwenyewe kwa manufaa ya mtu mwingine hutuleta karibu na Mungu, Chimbuko la uzima na u-milele, na kwa hiyo hutufanya tuwe na furaha zaidi.

Bwana mfufuka, ambaye, kulingana na ahadi yake dhahiri, anakaa pamoja na wafuasi wake siku zote hadi mwisho wa dunia (Mt. 28, 20), na atujalie sisi, wenye dhambi na wadhaifu, lakini wenye kiu ya kutafuta haki na ya kutaka wokovu, kurithi maisha ya furaha katika mwisho wa njia za dunia, ili mbinguni, ambako kuna makao yaliyoandaliwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu (Mt. 25, 34), tukaishi pamoja na watakatifu, katika uzima wa milele, wa utukufu wa utawala wake (Mtakatifu. Ambrosi Mediolanski: Wimbo “Tunamsifu Mungu kwako”).

Kanisa daima huhubiri juu ya furaha hii ya kungojea Ufalme ujao wa upendo, wakati Mungu atakuwa yote katika yote (1 Kor. 15, 28), hasa katika siku zenye kung’aa.za sherehe ya Pasaka.

Hebu na tuitii sauti yake iokoayo, ikituita kwa kinywa cha Mtume Paulo kusherehekea Pasaka si kwa chachu ya kale, si kwa chachu ya uovu na udanganyifu, bali kwa mkate usiotiwa chachu, wa usafi na kweli (1Kor. 5, 8). Hebu tuzingatie na tujaribu kuishi kulingana na Amri Takatifu, Neno la ukweli wa injili na matendo mema, tukiwashuhudia jirani zetu kwa maisha yetu yote na kwa wale walio mbali, kwamba Kristo amefufuka kweli, utukufu wote, adhama na heshima ni vyake Yeye milele na milele. Amina.

+PATRIARKI  WA  MOSKO  NA URUSI YOTE

Pasaka ya Kristo

2023

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu