Mnamo Septemba 22, 2023, Ofisi ya Jumba la Urusi mjini Dar es Salaam, Tanzania, iliendesha tamasha la uelimishaji wa kiroho – “Afrika ya Kiothodoksi”.
Washiriki wa hafla hiyo – wawakilishi wa madhehebu na imani tofauti – tofauti walikusanyika katika ukumbi wa Jumba la Urusi ili kujadili namna ya kuishi kwa utangamano, amani na uvumilivu kati ya watu wenye imani tofauti, na jinsi serikali inavyoweza kusukuma mbele mchakato wa kuunda mfumo wa maisha ya umoja wa madhehebu nchini, kuzuia mwelekeo wa malezi na mafundisho ya maadili-potofu pamoja na dhana ya kutovumiliana kiroho.
Ratiba ya tamasha ilijumuisha kutembelea maonyesho ya ikoni za Kiothodoksi na pia kutazama filamu ya kisanii ya Kirusi “The Tsar” (iliyoongozwa na P. Lungin, mwaka 2009).
Hafla hiyo ilifunguliwa na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Tanzania Mh. Andrei Avetisyan, ambapo hotuba yake ilifuatiwa na jumbe za salamu kutoka kwa Askofu Mkuu wa Afrika Metropolitani wa Klin Leonid na pia Metropolitani wa Tashkenti na Uzbekistani Vikenti, wakiwahutubia waalikwa kwa njia ya video.
Mwakilishi wa Muungano rasmi wa madhehebu za Tanzania, Sheikh Kundecha na kasisi wa Esarkia ya Kipatriarki nchini Tanzania, Mkuu wa Kituo cha Elimu, Padri Konstantin, pia walihutubia hadhara hiyo.
“Hatuna budi kuzuia mifarakano ya kidini, mashambulizi na mateso kwa waumini na viongozi wa dini, na pia kwa pamoja kuweka mazingira muafaka ya kiroho na yenye staha na heshima kwa hisia za kidini za wananchi wenzao” – ni wito uliotolewa na viongozi hao katika salamu zao, tovuti ya Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania inaripoti.
Askofu Mkuu wa Esarkia ya Afrika