Mwenyekiti wa Idara ya Misioni atembelea Kituo cha Elimu cha Esarkia kilichopo Kisarawe (Tanzania) - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Mwenyekiti wa Idara ya Misioni atembelea Kituo cha Elimu cha Esarkia kilichopo Kisarawe (Tanzania)

Jioni ya Aprili 13, 2023, usiku wa kuamkia Ijumaa Kuu ya Wiki Takatifu, mwenyekiti wa Idara ya Misioni ya Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika, Padri Georgi Maksimov, alitembelea Kituo cha Elimu cha Esarkia kilichopo Kisarawe (Tanzania).

Hivi sasa, pale shuleni wanasoma vijana 16 kutoka katika familia za Waothodoksi, zikiwamo  familia za makasisi. Kituo hicho kinaongozwa na kasisi wa Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika, Padri Konstantin Shoki.

Akiwa pamoja na makasisi wa Esarkia, na pia wanafunzi wa kituo hicho, Padri Georgi aliendesha ibada ya Alfajiri ya Kisigino Kikuu na usomaji wa Masomo 12, ya Injili, ya Mateso Matakatifu ya Bwana wetu Yesu Kristo.

 “Inafurahisha kuona watoto hao wanaifahamu vyema huduma ya ibada takatifu, waliisoma wakati wa ibada, katika lugha ya Kirusi, waliyojifunza katika Kituo cha Sayansi na Utamaduni cha Urusi kilichopo Dar es Salaam, Askofu Mkuu Metropolitani wa Klin Leonid alibainisha. katika ukurasa wake wa mtandao wa telegram.

 Baada ya ibada, Padri Georgi aliongea na wanafunzi, wakiwemo wale wanaotaka kuwa watawa, na pia akatembelea majengo ya makazi.

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu

-