Ujumbe wa Krismasi
Patriarchal Eksark ya Afrika ya Kanisa la Orthodox la Urusi,
Askofu Mkuu Konstantin wa Zaraisk.
Makasisi na waumini wote wa,
Patriako Eksarketi ya Afrika ya Kanisa la Orthodox la Urusi
Wapendwa Makasisi, na ndugu wote katika Kristo.
Ninawapongeza kwa moyo wangu wote katika Sikukuu hii ya Kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo!
Kanisa linatukumbusha katika nyimbo zake za Kiliturgia linatutangazia kwamba Kuzaliwa kwa Mwokozi kulidhihirisha Ukweli kwa ulimwengu wote na fursa ya kuufahamu Ukweli huo.
Jambo kuu ni kwamba Mungu alijidhihirisha kwetu kama Mungu-mtu yaani Mungu kweli na Binadamu kweli asiye na dhambi. Tangu mwanzo kabisa wa utumishi Wake kwa watu, Kristo alionyesha upole na unyenyekevu, na hakuzaliwa katika jumba la kifalme, bali alizaliwa katika pango ambamo mifugo walihifadhiwa.
Wachungaji wa mifungo ndiyo waliokuwa watu wa kwanza kutoka sehemu za mbali na sehemu za karibu, kuja kumwabudu Kristo, wakimletea zawadi kwa moyo safi. Kuja kwao kutoka mbali mjini na vijijini walifuatwa na watu wenye ujuzi wa maarifa, ambao ni Mamajusi. Walikuja kwa Mfalme wa Mbinguni na zawadi za thamani sana. Nasi tukisimama sasa mbele ya Kristo kama wachungaji na watu wenye hekima, sisi pia tutamletea zawadi za upendo wetu. Kristo anatuambia katika Injili ya Yohana 14:23 “Yeyote anipendaye atalishika neno langu,” Hivyo, Yeyote anayempenda Kristo anajaribu maishani mwake kutimiza yale anayotufundisha Kristo. Anatufundisha kuishi kulingana na dhamiri zetu na kuwa karibu zaidi na Mungu na majirani zetu. Anatufundisha tuwe wanyoofu, tuwasaidie wengine, tusiwe na kinyongo na mtu yeyote, tusiwe na wivu. Anakufundisha kuvumilia magumu ya maisha na kuwapa wengine uchangamfu wa mioyo yao. Lakini Yeye Kristo hafundishi tu, bali Yeye mwenyewe anatupa mfano wa maisha Yake na nguvu za kutimiza Amri Zake.
Bwana aliyezaliwa atutie nguvu sote katika upendo na maisha kadiri ya Injili inavyotufundisha.
Nawatakia wote msaada wa Mungu katika maisha na kazi zenu.
Naomba baraka za Mungu ziwe juu yanu.
Askofu Mkuu Konstantin wa Zaraisk,
Patriako Eksark wa Afrika.
Kanisa la Orthodox la Urusi