Makasisi wa Esarkia ya Kipatriarki washiriki ibada ya Pasaka katika Kanisa la Utatu Mtakatifu kule Vorobyovii Gori mjini Mosko - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Makasisi wa Esarkia ya Kipatriarki washiriki ibada ya Pasaka katika Kanisa la Utatu Mtakatifu kule Vorobyovii Gori mjini Mosko

Usiku wa Aprili 15-16, 2023, katika maadhimisho ya sikukuu ya Ufufuo Mtukufu wa Kristo, katika kanisa la Utatu Mtakatifu kule Vorobyovii Gori mjini Mosko, paroko wa kanisa hilo Kasisi Mkuu Andrei Novikov aliendesha ibada ya Alfajiri ya Pasaka na Liturgia takatifu.

Alihudumu pamoja na: makasisi wa kanisa hilo, na pia makasisi wa Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika: Padri Aleksei (Madagaska), Padri Boris (Togo), Shemasi Mtawa Kleonik (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo).

Wakati wa Liturgia, Injili ya Pasaka ilisomwa katika lugha ya Kislavoni cha Kanisa, Kigiriki, Kiingereza na Kifaransa.

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu