Mnamo Septemba 25, 2023, katika viwanja vya Kanisa la Watakatifu Wote pale Kulishki, Mosko, Askofu Mkuu wa Afrika, Metropolitani wa Klin Leonid, alikutana na Daudi Kwin, “askofu” wa kanisa lisilo rasmi la Kameruni.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na mwenyekiti wa Idara ya Misioni ya Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika, Padri Georgi Maksimov.
“Daudi alikuja Urusi kulitafuta Kanisa la Kiothodoksi la Urusi,” Metropolitani Leonid aliandika katika ukurasa wake wa “telegram”.
Katika “dayosisi ya Daudi Kwin kuna mapadri ishirini, watawa, waseminari, parokia saba, monasteri pamoja na kanisa kuu linaloendelea kujengwa mjini Duala, pamoja na zaidi ya waumini elfu moja.” Anasema kwamba wengi wa jamii yake wamefadhaishwa na hali mbaya ya maadili iliyoenea katika mamlaka kuu ya kanisa hilo lisilo rasmi, lenye makao makuu nchini Ufaransa. Wanatafuta Kanisa la kweli -lenye utamaduni thabiti wa kitume na kibiblia,” askofu huyo aliongeza.
Na akageukia mada-husika! “Katika mkutano wa leo, tulijadili hatua madhubuti za kuanzisha mafunzo ya katekisimu kamili kwa jamii hii, ili kwamba, baada ya kukamilika kwake, kwa mafanikio, swala la kuwapokea katika Kanisa la Kiothodoksi la Urusi litashughulikiwa,” alihitimisha Baba Askofu.
Askofu Mkuu wa Esarkia ya Afrika