Mafunzo ya kawaida kwa makasisi na walei wa Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika yakamilika - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Mafunzo ya kawaida kwa makasisi na walei wa Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika yakamilika

Mafunzo ya kawaida kwa makasisi na walei wa Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika yakamilika.

Mmisionari A.V. Lyulka alitoa mihadhara juu ya Maandiko Matakatifu na Katekisimu katika majimbo yote tisa ya Kenya, mkazo maalum ukiwekwa katika masuala ya eklezia na skismolojia, sakramenti za Ubatizo na Toba katika maisha ya mkristo.

Kwa ujumla, madarasa yaliendeshwa katika parokia 22, na mihadhara ilihudhuriwa na watu 916 – mapadri 52 na walei 864. Utaratibu huo wa mafunzo ulionekana kupendwa sana, makasisi na waumini wakimkaribisha mwalimu kwa bashasha na kuonyesha shukrani zao kwa Uongozi wa Kanisa la Othodoksi la Urusi.

Kwa mujibu wa Metropolinani wa Klin Askofu Mkuu Leonid, ili kuifikia hadhira pana zaidi, unaandaliwa utaratibu wa kuzindua moduli ya elimu kwa njia ya mtandao.

Utaratibu huo hivi sasa unatumika nchini Rwanda.

Askofu Mkuu wa Esarkia ya Afrika

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu