Ujumbe wa Krismasi
wa Patriarka Kirill wa Mosko na Urusi Yote
kwa wachungaji-wakuu, wachungaji, mashemasi,watawa
na waumini wote wa Kanisa la Kiothodoksi la Urusi
Wachungaji-wakuu wapendwa wa Bwana, Waheshimiwa Makasisi na Mashemasi, Watawa wapenda-Mungu, wapendwa kaka na dada zangu!
Upendo wa Mungu, usioelezeka, umetukusanya leo ili, katika umoja wa roho na ushirika wa amani (Efe. 4:3) kusherehekea moja ya maadhimisho makubwa kabisa, na ambayo ni kati ya Siku kuu tukufu za Kanisa – Kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Nikitukuza ujio wa Mwokozi duniani, ninawapongeza, kwa moyo wa wote, wapendwa wangu, kwa tukio hili la furaha, ambalo lilifungua enzi mpya katika uhusiano kati ya Mungu na watu wake.
Kila tunapotazama yaliyotokea milenia mbili zilizopita, tunajaribu kufahamu ukubwa wa muujiza wa Umwilisho wa Mungu na hatukomi kushangazwa na wema pamoja na huruma ya Muumba wetu. Kwa karne nyingi, wanadamu wallchoka katika kumtazamia Mpatanishi aliyeahidiwa na Bwana ( Mwa. 49:10 ): Mfalme mwenye haki na mwenye wokovu ( Zek. 9:9 ), ambaye katika Jina lake mataifa yataweka tumaini lao ( Isa. 42 ; 4). Na kwa hiyo, wakati wa utimilifu ulipofika, Mtoto alizaliwa kwetu (Isaya 9:6), ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele (Yohana 3:16). Upendo wa Mungu, upitao ufahamu (Efe. 3:19), ulituma ulimwenguni si mtetezi, wala malaika, si mtawala mwenye nguvu na mamlaka, kama watu walivyofikiri – bali Mungu Mwenyewe alifanyika mwili ili kumkomboa mwanadamu kutoka kwenye nguvu za dhambi. na uovu.
Inashangaza kwamba tukio kubwa zaidi katika historia, ambalo lilitangazwa na manabii wa Agano la Kale, na ambalo hata wanafalsafa mashuhuri wa mambo ya kale walitabiri, lilitokea kwa unyenyekevu kiasi kwamba hata kwa nje halikujidhihirisha. Bethlehemu ilikuwa imelala, Yerusalemu ilikuwa imelala. Yuda yote ilikuwa imelala. Bwana Mwenyezi—Mfalme wa Wafalme na Mtawala wa ulimwengu, alionekana katika ulimwengu, si kwa sauti kuu za tarumbeta (Zab. 150, 3) na furaha ya ulimwengu wote, bali kwa unyenyekevu na upole, katika ukimya wa pango la huzuni, usiku, akiimbiwa nyimbo za kubembeleza, na jeshi la malaika pamoja na wachungaji wachache waliokuja kushuhudia kilichotokea (Lk. 2, 15).
Mwanzoni kabisa mwa safari yake ya hapa duniani, Bwana alitaka “kuonyesha, katika mipaka ya kujishusha kabisa, sura ya wema -” Mtakatifu Yohana Zlatust anatufikirisha.Upendo mkamilifu pekee, ndio unaotenda kwa wema, upendo ambao haujitafutii mambo yake pekee (1 Wakorintho 13:4-5), haujivuni wala haudai heshima na utukufu, bali uko tayari kustahimili shida na huzuni zote, kwa manufaa ya wengine. “Ni kwa sababu hiyo,” mwalimu wa kiekumeni ya Kanisa anaendelea kusema, “Bwana anauchukua mwili wangu ili niweze kuingiza Neno lake, na akiisha kuuchukua mwili wangu, atanipa Roho Wake ili, kwa kutoa na kupokea, aweze kunijulisha.hazina ya uzima” (Ujumbe wa Krismasi). Katika hili, upendo mwingi wa Mungu ulidhihirishwa kwetu, kwamba tulipokea hazina ya kweli ya uzima – Mungu Mwenyewe, Ambaye kwa Yeye vitu vyote vilitoka, na Kwake vitu vyote (Rum. 11:36).
Upendo – ndio sababu halisi na nguvu inayosukuma matendo Matakatifu. Aliileta dunia na akamuumba mwanadamu, kwa ukarimu akamtunuku zawadi. Kwa upendo, anakuja kumwokoa alipoanguka na kupoteza mawasiliano na Muumba wake. Kulingana na kusudi la Mungu Muumba, mantiki ya maisha ya mwanadamu ni kwamba sisi pia tupendane – sisi kwa sisi (Yohana 14:34). Lakini hili linaweza kufikiwaje katika ulimwengu huu ambamo kuna uovu mwingi pamoja na chuki? Ili kufanya hivyo, kwanza kabisa ni lazima kufungua na kuutoa moyo wako kwa Mungu. Ni Yeye pekee awezaye kuubadilisha na kuupanua, kwani pamoja na kwamba hivi sasa ni dhaifu sana na uliosongwa, na kuupatia uwezo wa kukumbatia walio karibu na walio mbali, na pia wale wanaotenda mema na hata wanaotuudhi – wale wote ambao tumeitwa kuwapenda, kulingana na amri ya Kristo. , tukimwiga Baba yetu wa Mbinguni kikamilifu ( Mathayo 5:48 ).
Tunapoinama kwa maombi mbele ya Mtoto mchanga aliyezaliwa, hebu tufikirie, ni zawadi gani tutatoa kwa Bwana wa Ulimwengu? Je, kunaweza kuwa na kitu chochote kinachostahili na kinacholingana na ukuu wa Muumba wa Milele? Ndiyo, kuna zawadi ya thamani sana ambayo Bwana anatamani zaidi ya yote: mioyo yetu minyenyekevu, upendo na huruma. Hebu tumtukuze Kristo aliyefanyika mwili, si tu kwa nyimbo nzuri na jumbe za pongezi, bali zaidi ya yote, kwa matendo mema. Tutashiriki furaha angavu ya Krismasi na wale wanaohitaji, tuwatie joto majirani zetu kwa utunzaji wetu, tutembelee wagonjwa na wenye kulemewa na huzuni. Tuwafariji na tuwategemeze wale waliokata tamaa, na tuwafunike kwa sala, wote wale walio katika machafuko na huzuni. Nguvu kuu ya wokovu iliyomo katika upendo, huondoa hali ya kutokujali pamoja na uovu, huondoa chuki na hasira. Inapunguza hisia za ujeuri katika mioyo ya watu na hurekebisha mapindo mengi ya mahusiano katika jamii! Tukiwa tunaishi kwa kuyafanyia kazi haya, tutatimiza kweli ya wito wetu wa Kikristo, kwani kwa kumiminiwa upendo huku, kunalingana na neno la Mtakatifu Isaka Sirin, tunafanana na Mungu (Maneno ya kujikinai. 48). Fumbo la Umwilisho wa Mungu, ni fumbo la uwepo halisi wa Mungu hapa duniani. Mtume na mwinjilisti Yohana, akiyaona wazi maisha ya karne inayofuata, anashuhudia juu ya Bwana kuishi kikamilifu na watu: “Naye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake, na Mungu mwenyewe atakuwa Mungu wao” (Ufu 21:3). Hata hivyo, fumbo hili, lisiloweza kutamkwa, la uwepo wa Mungu hapa dunianui, linaanza kubainika kwa Kuzaliwa kwa Mwokozi, wakati ulitimia na Ufalme wa mbinguni ukakaribia (Marko 1:15). Tunaingia kwa uwazi katika ukweli huu, huku tukiunda Kanisa Moja Takatifu la Kristo, ambalo, kupitia hilo, sisi sote, wapendwa wangu, ni wajumbe na wawakilishi wa Ufalme huu Mkuu, wa upendo. Uzoefu huu wa ajabu na wa kina wa “Mungu yu pamoja nasi” ni kiini cha maisha ya ajabu, ya ndani ya Kanisa. Tukumbuke kwamba, ikiwa Mwenyezi Mwenyewe – Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho ( Ufu. 22:13 ) – aliikumbatia historia ya mwanadamu na kuahidi kukaa nasi siku zote hadi mwisho wa dahari. ( Mathayo 28:20 ), basi hatuna chochote cha kuogopa na kuhoia hali zinazosumbua katika nyakati hizi. Tuitikie upendo mkuu wa Mwokozi, na tujifunze kujikabidhi kikamilifu kwa Bwana, na kutumaini majaliwa yake mema, ili tutoe ushuhuda, kwa ujasiri, na kufurahi hadi Ujio wa Pili wa utukufu wa Kristo, hata mwisho wa dunia ( Isaya 8:9 )
Mungu yu pamoja nasi!
PATRIARKA WA MOSKO NA URUSI ZOTE
Krismasi 2023/2024
Mosko