Ujumbe wa Krismasi
kutoka kwa Askofu wa Zaraisk Konstantin,
Kaimu Askofu Mkuu wa Afrika
kwa mapadri, watawa na waumini wote wa Esarkia
ya Afrika ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi
Wapendwa Baba, Kaka na Dada zangu katika Kristo!
Ninawapongeza, kwa moyo mkunjufu, kwa Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Kristo!
Tulikuwa tukilingojea tukio hili kwa hamu kubwa, tukijiandaa. Sasa imekuja.
“Kristo amezaliwa – msifuni! Kristo kutoka mbinguni – mpokeeni!” anatuita sisi tulio Kanisa takatifu .
Muujiza usioelezeka umefanyika: Mungu wa milele amekuwa Mwanadamu. Mwana wa Mungu, Bwana Yesu Kristo, amekuja kwetu ili kutusafisha, kutuponya na kutufungulia njia ya kuelekea kwenye Ufalme wa mbinguni. Kristo ametuletea wokovu na uzima wa milele.
Tutamlakije?
Tumsalimu Mtoto Kristo kwa ibada yenye furaha na taratibu stahiki za Krismasi. Tujisahihishe na tujaribu kuwa wasikivu na wepesi wa kukutana na mahitaji ya wapendwa wetu. Tumwombe Bwana aingie katika maisha yetu na kuyabadilisha.
Na tumpe Kristo kibali cha kushughuluka na maisha yetu, ayaongoze, awe ngao yetu, sawasawa na Neno la Bwana: “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima” (Yohana 14:16).
Hebu tumfuate Kristo na tuishi kwa uaminifu, kwa usahihi, Kikristo, tukifuata amri za Mungu, kwa amani na upendo kwa majirani zetu.
Ninawatakia nyote msaada wa Mungu katika maisha na kazi, faraja na rehema kutoka kwa Mwokozi Aliyezaliwa.
Ninawaombea baraka za Mungu ziwamiminikie!
Askofu wa Zaraisk Konstantin,
Kasisi wa Patriarkia ya Mosko na Urusi Yote,
Kaimu Askofu Mkuu wa Afrika
Kismasi
2023/2024