Mnamo Septemba 29, 2023, katika Ubalozi wa Jamhuri ya Morisi katika Shirikisho la Urusi, kulifanyika mkutano kati ya Mwenyekiti wa Idara ya Misioni ya Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika, Padri Georgi Maksimov na Balozi wa Morisi nchini Urusi, Mh.Hesvari Janke.
Mkutano huo ulifanyika katika mazingira ya urafiki na maelewano, Askofu Mkuu Metropolitani wa Klin Leonid aliainisha katika ukurasa wake wa “telegram”.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Kasisi Mkuu Dimitri Matienko ambaye anatarajia kwenda Morisi kwa ajili ya kufanya kazi nchini humo na kushughulikia masuala ya uanzishaji wa parokia pamoja na huduma zake.
Pande hizi mbili zilijadili swala la usajili wa Esarkia nchini Morisi na ufundishaji wa misingi ya imani ya Kiothodoksi katika “Shule ya Dini”, taasisi inayounganisha imani zote za asili za nchi hii.
Mheshimiwa Janke alisema kwamba Kanisa la Kiothodoksi la Urusi litaweza kutengewa kipande cha ardhi, bila malipo yoyote kwa serikali, kwa ajili ya ujenzi wa hekalu, na akatoa uthibitisho kwamba misioni ya Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika, ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi, na shughuli zake zote zitaungwa mkono kikamilifu.
Askofu Mkuu wa Esarkia ya Afrika