Balozi wa Benin nchini Urusi akutana na kasisi wa Esarkia ya Afrika - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Balozi wa Benin nchini Urusi akutana na kasisi wa Esarkia ya Afrika

Mnamo tarehe 10 Mei, 2023, Balozi wa Jamhuri ya Benin katika Shirikisho la Urusi, Mh. Akambi Andre Okunlola-Biau, alikutana na kasisi wa Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika, Padri Parfeni Dansu, mjini Mosko.

“Mheshimiwa Balozi amekaribisha sana ujio wa Kanisa la Kiothodoksi la Urusi nchini Benin, na amekiri kuwa furaha yake imekolezwa zaidi na ile hali kwamba taarifa hii ameipata kutoka kwa mwananchi mwenzake, na hivyo akasema kuwa, kwa upande wake, yuko tayari kushirikiana na Askofu Mkuu wa Afrika na kwamba atafanya kila linalowezekana.kusaidia huduma yetu ya misioni,” aliandika Metropolitani wa Klin Leonid, katika ukurasa wake  wa “telegram”. “Tunapokea maombi kutoka kwa waumini nchini Benin, ya kufungua parokia za Kanisa la Kiothodoksi la Urusi nchini humo, nasi tutachukua hatua katika mwelekeo huo.”

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mshauri wa Ubalozi- Giono Morel Gbenakpon Nami, mwenyekiti wa Idara ya Misioni ya Esarkia Padri Georgi Maksimov na Konstantin Gorditsa, anayehusika na  masuala ya wanafunzi wa kigeni.

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu