Mnamo Agosti 14, 2023, kule mjini Minsk, Askofu Mkuu wa Belarus Yote – Metropolitani wa Minsk na Zaslavski Benyamini, alikutana na wanafunzi kutoka nchi za Afrika wanaosoma katika Chuo cha Theolojia cha St. Petersburg.
Wakati wa mkutano huo, wanafunzi walieleza kuhusu historia na hali ya sasa ya maisha ya Kanisa katika bara la Afrika na wakaelezea hisia zao baada ya kuzuru Jamhuri ya Belarusi.
Katika ziara yao katika ardhi ya Belarusi, wanafunzi walifahamiana na mahekalu matakatifu ya jiji la Minsk na walifanya mazungumzo na vijana wa Kiothodoksi waliokuwa kwenye kambi ya mapumziko, ya majira ya joto, ya Kanisa Kuu la Petro na Paulo la Minski.
Tovuti rasmi ya BPC