Sinodi  Takatifu  yasisitiza  umuhimu  wa  miradi  ya  pamoja  ya Kanisa la Kiothodoksi  la Urusi  na Kanisa  la  Ethiopia - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Sinodi  Takatifu  yasisitiza  umuhimu  wa  miradi  ya  pamoja  ya Kanisa la Kiothodoksi  la Urusi  na Kanisa  la  Ethiopia

Mnamo Machi 16, 2023, katika mkutano wa Sinodi Takatifu, Metropolitani wa Volokolamsk Antoni, Mwenyekiti wa Idara ya Mahusiano ya Kanisa na Taasisi za Nje, aliwasilisha ripoti ya mkutano wa pili wa Tume ya Mazungumzo ya Pande Mbili, kati ya Kanisa la  Kiothodoksi la Urusi na Kanisa la Ethiopia. (jarida No. 17).

Wajumbe wa Sinodi walionyesha kuridhishwa na mafanikio ya kazi iliyofanywa  na Tume, na wakasisitiza umuhimu wa miradi ya pande hizi mbili, ambayo ni pamoja na:

• hatua za pamoja katika kuwalinda Wakristo;

• kushirikiana katika hoja kwenye majukwaa ya kimataifa;

• ksaidiana katika kulinda maadili ya kitamaduni;

• kubadilishana uzoefu katika  uwanda  wa vyombo vya habari;

• msaada wa kichungaji kwa watu wa nchi  moja wanaoishi katika  nchi – mwenza ( Ethiopia na Urusi); ushirikiano katika diaspora;

• mawasiliano kati ya wawakilishi wa utawa, na uendelezaji  wa programu za hija;

• ushirikiano katika nyanja za masomo, kijamii, kanisa-viwanda na maswala ya vijana.

                                                                ***

Kuanzia Februari 11 hadi 16, 2023, mkutano wa pili wa Tume ya Mazungumzo ya Pande Mbili, kati ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi na Kanisa la Ethiopia ulifanyika kule Mosko.

Ujumbe kutoka Patriarkia ya Mosko uliundwa na: Metropolitani wa Klin Leonid, Mwenyekiti-Mwenza wa Tume; Kasisi- Mtawa Stefan (Igumnov), Katibu wa DECR kwa Mahusiano kati ya Wakristo, Katibu wa Tume; V.V. Kipshidze, Makamu Mwenyekiti wa Idara ya Mahusiano ya Kanisa na Vyombo vya Habari; Shemasi Dimitri Serov, Mkurugenzi wa Shirika la Uchapishaji la Chuo cha Theolojia cha Mosko.

Miongoni mwa washiriki kutoka Kanisa la Ethiopia walikuwa: Mkuu wa Chuo cha Theolojia cha Utatu Mtakatifu cha Addis Ababa, Askofu Mkuu wa Omo Kusini Abuna Filipos – Mwenyekiti-Mwenza wa Tume; Mkurgenzi wa Idara ya Mahusiano ya Kanisa na Taasisi za Nje, Padri Danieli Seifemihael – Katibu wa Tume; Mkurugenzi wa Idara ya Miradi ya Kanisa, Mkuu wa parokia za Addis Ababa, Kasisi Mkuu Weldejesus Sefugalato.

Makubaliano ya kuundwa kwa Tume yalifikiwa kati ya Patriarki Mtakatifu wa Mosko na Urusi Yote Kirill  na Patriarki Mtakatifu wa Ethiopia  Abuna Matias   wakati wa ziara ya Mkuu huyo wa Kanisa la Ethiopia nchini Urusi, iliyofanyika kuanzia tarehe 15 hadi 20 Mei, 2018.

Tume ilifanya tathmin ya kazi yake tangu mkutano wake wa awali uliofanyika Januari 21-25, 2019  kule Addis Ababa. Licha ya kupitia kipindi chenye vikwazo vya karantini na changamoto  nyingi nyingine, mipango kadhaa ya pande hizi mbili imetekelezwa kwa mafanikio makubwa. Tume iliwasilisha mapendekezo ya kuendeleza zaidi ushirikiano katika maeneo muafaka. Miongoni mwake yakiwa: juhudi za pamoja katika kuwalinda Wakristo; kushirikiana katika hoja kwenye majukwaa ya kimataifa; kusaidiana katika  kulinda maadili ya kitamaduni; kubadilishana uzoefu katika uwanda wa vyombo vya habari; kutoa msaada  wa kichungaji  kwa watu wa nchi za Ethiopia na Urusi (wanaoishi katika mojawapo kati ya nchi hizi au nyingine); ushirikiano katika nchi-mtawanyiko (diaspora); kukuza mawasiliano kati ya wawakilishi wa utawa, na muendelezo  wa programu za hija; ushirikiano katika nyanja za masomo, huduma za kijamii, kanisa-viwanda na maswala ya vijana.

Mnamo Februari 14, kwa baraka za Patriarki Mtakatifu Kirill, Metropolitani wa Volokolamsk  Antoni, Mwenyekiti wa Idara ya Mahusiano ya Kanisa na Taasisi za Nje, alikutana na ujumbe wa Kanisa la Ethiopia. Kwa niaba ya Patriarki Mtakatifu wa Ethiopia na Sinodi ya Kanisa la Ethiopia, Abuna Matias, kiongozi wa ujumbe, Askofu Mkuu Abuna Filipos, alishukuru kwa msaada ambao Patriarkia  ya Mosko ilitoa kwa Kanisa la Ethiopia wakati wa jaribio  la hivi karibuni la kikundi cha waasi kutaka kufanya mpasuko wa kanisa nchini Ethiopia. Kwa upande wake, Metropolitani Antoni alitoa shukrani kwa msaada unaoendelea kutolewa na Kanisa la Ethiopia katika maeneo ya Wakristo, katika kukabiliana na njama mbalimbali  za ubaguzi zinazofanywa dhidi ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi.

Mkutano mwingine wa Tume umepangwa kufanyika mwaka 2024 nchini Ethiopia.

Shirikisha katika mitandao ya kijamii:

Taarifa zote zilizo na maneno muhimu

-