Safari ya mwenyekiti wa Idara ya Kimisionari ya Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi kutoka Esarkia ya Africa, Padri George Maximov, kwenda Angola imekamilika.
Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi Mnamo tarehe 18 Juni, 2023, katika Wiki ya Watakatifu Wote waliong’aa katika ardhi ya Urusi, katika ukumbi wa shule ya Kirusi katika mji mkuu wa Angola, Luanda, Padre George alifanya ibada ya misa, ambapo Warusi wanaoishi nje ya urusi walipata. sakramenti ya kitubio na Komunio na pia waliwakumbuka jamaa na marafiki zao. Siku moja kabla, Padre George alikutana na Balozi Mdogo wa Urusi Angola V.N. Tararov, pamoja na Warusi wanaoishi nchini Agola. Matarajio ya kuanzisha uwepo wa kudumu wa Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi nchini Angola yalijadiliwa. Katika safari hiyo, Padre. George alikutana na kiongozi na wawakilishi wa mtaa, kundi lisilo rasmi la Orthodoksi, ambalo linaomba kuandikishwa ili kuwa sehemu ya Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi. Makubaliano yalifikiwa kuanza mchakato huo. “Ninatoa shukrani zangu kwa Balozi wa Shirikisho la Urusi katika Jamhuri ya Angola V.N. Tararov kwa makaribisho mazuri na usaidizi katika kuandaa safari ya kikazi ya mwakilishi wa Baba Askofu wa Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi katika Esarkia ya Afrika” Leonid Metropolitan wa Klin aliandika katika ukurasa wake wa telegramu.