Kwa ajili ya jambo hili, mmisionari A.V. Lyulka aliizuru Gabon na kufanya mihadhara ya katekisti katika parokia zote nne za jamii hiyo – kule Librevilli, Ntum na katika kijiji cha Abing Assi.
“Waumini walisikiliza mihadhara kwa shauku kubwa, wakaelewa tofauti kati ya Uothodoksi, Ukatoliki na Uprotestanti, waliuliza maswali, wakaomba kupatiwa vitabu – inafurahisha kushuhudia shauku kama hiyo ya kujifunza imani. Pamoja na mihadhara hiyo, Aleksanda Vyacheslavovich aliendesha warsha juu ya kusoma na kuimba kwa utaratibu wa Kanisa la Kiothodoksi la Urusi,” Metropolitani wa Klin Leonid alisema katika ukurasa wake wa “telegram”.