Usiku wa Aprili 15-16, 2023, katika maadhimisho ya sikukuu ya Ufufuo Mtukufu wa Kristo, katika kanisa la Utatu Mtakatifu kule Vorobyovii Gori mjini Mosko, paroko wa kanisa hilo Kasisi Mkuu Andrei Novikov aliendesha ibada ya Alfajiri ya Pasaka na Liturgia takatifu.
Alihudumu pamoja na: makasisi wa kanisa hilo, na pia makasisi wa Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika: Padri Aleksei (Madagaska), Padri Boris (Togo), Shemasi Mtawa Kleonik (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo).
Wakati wa Liturgia, Injili ya Pasaka ilisomwa katika lugha ya Kislavoni cha Kanisa, Kigiriki, Kiingereza na Kifaransa.