Mnamo Machi 18, 2023, “Redio Sputnik” ilitangaza taarifa ndefu kuhusu Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika “Afrika. Kurejea“.
Walioshiriki katika kuandaa taarifa hiyo ni: Askofu Mkuu wa Afrika Metropolitani wa Klin Leonid, Paroko Andrei Novikov, Dekani wa parokia za Esarkia nchini Nigeria-Kasisi Mkuu Nifont (Ule), Mwenyekiti wa Idara ya Misioni Padri Georgi Maksimov, Padri Georgi Chabvera (Malawi),Mtawa Matrona Jepchirchir (Kenya).
Rekodi ya tangazo hilo inapatikana kwenye tovuti ya “Redio Sputnik”, kwa kiunganishi.
Waandaaji wa taarifa hiyo wameeleza kuhusu hali ya Wakristo wa Kiothodoksi barani Afrika ilivyokuwa, na jinsi maisha yao yalivyobadilika kufuatia ujio wa misioni ya Esarkia, kwa nini barabara kuu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ilipewa jina “Urusi”, na jinsi Waafrika wanavyomuunga mkono Rais Vladimir Putin.