Patriarki Mtakatifu Kirill ampongeza Askofu mkuu Leonid wa Klin kwenye kumbukumbu ya miaka 10 ya kuwekwa wakfu kwake - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Patriarki Mtakatifu Kirill ampongeza Askofu mkuu Leonid wa Klin kwenye kumbukumbu ya miaka 10 ya kuwekwa wakfu kwake

Patriarki Mtakatifu Kirill wa Moscow na Urusi yote amempongeza Askofu mkuu wa Africa Metropolitani Leonid wa Klin kwenye kumbukumbu ya miaka 10 ya kuwekwa wakfu kwake kuwa Askofu.

“Inafurahisha kushuhudia kwamba kwa muda mrefu umejaribu mara kwa mara kwa uangalifu na uwajibikaji kutimiza kwa utii kila jambo liliowekwa juu yako katika Ukuhani. Miaka kumi iliyopita, kwa mapenzi ya Mungu, wema na ukamilifu (Rum. 12:2), uliidhinishwa na kukubali hadhi ya Uaskofu,” ujumbe wa Patriarki Mtakatifu unasomeka hivyo.

“Sasa, kwa kuwatunza makasisi na kundi la Esarkia ya Kipatriaki ya Afrika na Dayosisi ya Yerevan-Armenia, unajitahidi kuendeleza maisha ya kanisa katika nchi ulizokabidhiwa, uwaangazie wenzetu kwa nuru ya imani ya Kristo, uwafundishe katika kweli za injili,” Patriarki Mtakatifu Kirill alibainisha na kumtakia “nguzu, msaada wa ukarimu wa Mungu na mafanikio katika siku zijazo kufanya kazi kwa manufaa ya Kanisa Takatifu.”

Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika

 

Shirikisha katika mitandao ya kijamii: