Mazoezi ya Kiliturgia kwa kundi la wanafunzi wa masomo ya ukasisi, wanaozungumza lugha ya Kifaransa, yahitimishwa - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Mazoezi ya Kiliturgia kwa kundi la wanafunzi wa masomo ya ukasisi, wanaozungumza lugha ya Kifaransa, yahitimishwa

Mafunzo ya darasani na pia mazoezi ya kiliturgia kwa kundi  la wanafunzi wa masomo ya ukasisi, wanaozungumza lugha ya Kifaransa, wa Esarkia ya Kipatriarki ya  Afrika, yamehitimishwa.

Mtihani wa mwisho ulifanywa jana.

Haya ni mahafali ya pili. Kundi  la kwanza  lilimaliza mafunzo ya darasani na kufanya mazoezi katika makanisa na nyumba za watawa za Kanisa la Kiothodoksi la Urusi mwishoni mwa mwaka 2022 – mwanzoni mwa 2023.

Hadi  kufikia leo, watu 12 kutoka nchi 8 za Afrika wamekwishapata ubarikio matakatifu wa Ukasisi na tayari wamerejea  katika  parokia zao, ambako wanaboresha na kuanzisha maisha ya kiroho kwa taratibu za Kanisa la Kiothodoksi la Urusi. Parokia za kwanza za Patriarkia ya Mosko zinaanzishwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Togo na pia Kodivaa (“Ivory Coast”).

“Kwa moyo mkunjufu, ninamshukuru sana Mwenyekiti wa Idara ya Misioni ya Sinodi Askofu Yutimius wa Luhovitski, pamoja na walimu, kwa ushirikiano mwema unaozaa matunda,” aliandika Askofu Mkuu wa  Afrika Metropolitani wa Klin Leonid , katika ukurasa wake  wa “telegram”.

       

Shirikisha katika mitandao ya kijamii: