Mtakatifu Patriarki Kirill atembelea Stendi ya Esarkia ya Kipatriarki ya Afrikka kwenye Mkutano wa kilele wa Urusi-Afrika - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Mtakatifu Patriarki Kirill atembelea Stendi ya Esarkia ya Kipatriarki ya Afrikka kwenye Mkutano wa kilele wa Urusi-Afrika

Mnamo Julai 27, 2023, Mtakatifu Patriarki Kirill wa Mosko na Urusi Yote alishiriki katika Mkutano wa kilele wa Pili wa Urusi—Afrika, uliofanyika St. Petersburg. Katika kongamano la Uchumi na Huduma za Kibinadamu  la Urusi – Afrika, lililofanyika pembezoni mwa Mkutano wa kilele ulioongozwa na Rais wa Shirikisho la Urusi V. V. Putin, Mkuu wa Kanisa la Kiothodoksi la Urusi alitoa hotuba iliyojikita katika maswala ya uhusiano wa Urusi na Afrika na pia misioni ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi katika bara la Afrika.

Siku hiyo hiyo, Mtakatifu Patriarki Kirill alitembelea stendi ya Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika, iliyoandaliwa katika eneo la mkutano huo. Askofu Mkuu wa Afrika, Metropolitani wa Klin Leonid, alitoa maelezo kwa Mtakatifu Patriarki juu ya yaliyokuwa yanaonyeshwa pale.

Mtakatifu Patriarki aliambatana na Metropolitani wa St. Petersburg na Ladoga  Varsonofi , Metropolitani wa Volokolamski Antoni, Mwenyekiti wa Idara ya Mahusiano ya Kanisa na nchi za Nje ya Patriarkia ya Mosko.

Kasisi Mkuu Aleksanda Tkachenko, kasisi wa Dayosisi ya St. Petersburg, mwanzilishi na mkurugenzi wa Hospitali ya watoto yenye uangalizi maalum kule St. Petersburg, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Misaada kwa Watoto wenye Magonjwa sugu “Jamii Njema”, Katibu Mahsusi wa Mtakatifu Patriarki Kirill Kasisi Mkuu-mtawa Aleksei (Turinkov), na makasisi wa Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika pia walitembelea stendi hiyo na kupatiwa maelezo juu ya maonyesho yaliyowasilishwa hapo.

Mtakatifu Patriarki Kirill alifurahia maonyesho ya picha yanayoelezea juu ya matukio ya kufurahisha sana katika maisha ya Esarkia na pia taswira ya elimu ya kiroho ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi kule Kampala, mji mkuu wa Jamhuri ya Uganda. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa Afrika Metropolitani Leonid, mradi huo unatekelezwa kwa ushiriki wa karibu wa  taasisi ya ANO “Baraza la Kikanda la Afrika Mashariki” linaloongozwa na rais wake – I.V. Shkarban.

Esarkia ya Kipatriaki ya Afrika iliundwa kwa mujibu wa azimio  la Sinodi Takatifu ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi la tarehe 29 Desemba 2021 (Jarida No. 100) ikiwa na Dayosisi ya Afrika Kaskazini na ya Kusini mwa Afrika. Katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu uliopita, esarkia  imefungua zaidi ya parokia 200 katika nchi 25 za Afrika.

Huduma ya Vyombo vya Habari ya Patriarkia ya Mosko na Urusi Yote

 

Shirikisha katika mitandao ya kijamii: