Mnamo Julai 19, 2023, Mkutano wa Maaskofu wa Kanisa la Kiothodoksi la Urusi ulifanyika katika Monasteri ya Utatu Mtakatifu ya Sergius, chini ya uenyekiti wa Mtakatifu Patriarki wa Mosko na Urusi Yote Kirill.
Mkutano huo wa Maaskofu uliitishwa kwa mujibu wa azimio lililopitishwa na Sinodi Takatifu ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi mnamo Desemba 29 (Jarida Na. 121): “Kwa ajili ya majadiliano ya kindugu kuhusu hali ya kanisa, kuitisha Mkutano wa Maaskofu Julai 19, 2023, utakaojumuisha dayosisi zote na maaskofu wa nchini Urusi, bila kukosa, na pia maaskofu wa nchi zingine – kwa kadri ya uwezekano wao kuja Mosko”.
Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Metropolitani wa Klin Leonid ambaye ni Askofu Mkuu wa Afrika.
Mtakatifu Patriarki Kirill alitoa hotuba kuu.
Metropolitani wa Hungaria na Budapesti Hilarioni, ambaye ni mwenyekiti wa Tume ya Kibiblia na Kitheolojia ya Sinodi, alitoa taarifa juu ya uandaaji wa hati “Juu ya kupotoshwa kwa Mafundisho ya Kiothodoksi kuhusu Kanisa, katika vitendo vya Patriarkia ya Konstantinopo pamoja na mihadhara ya wawakilishi wake”.
Mkuu wa Idara ya Sheria ya Patriarkia ya Mosko, Abbess Ksenia (Chernega), aliutaarifu mkutano kuhusu mabadiliko katika sheria juu ya madhehebu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Patriarkia ya Mosko, Metropolitani wa Ufufuo Dionisius aliandaa miniti za hitimisho la Mkutano.
Baada ya majadiliano hayo, lilipitishwa Azimio la Baraza la Maaskofu.
Kama ilivyoainishwa katika Azimio, “Mkutano wa Maaskofu unabainisha kwa masikitiko kwamba viongozi wa Patriarkia ya Konstantinopo, wamepofushwa na kiu ya kutaka kukidhi maslahi ya kibinafsi na tamaa, wamekuwa sehemu ya vyombo vya kisiasa vinavyochukia Uothodoksi. Baada ya kuzingatia hitimisho lililotolewa na Tume ya Kibiblia na Kitheolojia ya Sinodi “Juu ya Upotoshwaji wa Mafundisho ya Kiothodoksi kuhusu Kanisa, katika vitendo vya oungozi wa Konstantinopo pamoja na mihadhara ya wawakilishi wake,” washiriki wa Mkutano wa Maaskofu wanakubaliana na hitimisho hilo na utaliwasilisha kwenye Sinodi Takatifu kwa ajili ya kuidhinishwa”.
Askofu Mkuu wa Esarkia ya Afrika