“Hivi sasa, Esarkia ya Kipatriarkil ya Afrika ipo sana katika nchi 18 za bara hilo, na ni mwaka mmoja tu tangu kuanzishwa kwake kwa azimio la Sinodi Takatifu ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi,” Askofu Mkuu wa Afrika Metropolitani wa Klin Leonid alisema katika mahojiano na “TASS” Desemba 19, 2022.
“Mnamo tarehe 18 Desemba, upadirisho wa kwanza ulifanyika katika Kanisa la Ufufuo wa Kristo kule Rabat. Mfuasi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sergiy Voemava, aliwekewa mikono kuwa shemasi. Hivi majuzi alihitimu kozi ya theolojia kule Mosko. Sasa ana mzigo mkubwa wa kazi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati: anaendesha shule, ambayo tunasaidia kuijenga upya, na jumuiya nyingine tatu kubwa,” askofu alisema.
“Pia Jumapili, tulimwekea mikono Shemasi Herman Edianga kuwa Kasisi. Anatoka Uganda, nchi ambako nilifanya ziara yangu ya kwanza kama Askofu Mkuu wa Afrika,” Metropolitan Leonid aliongeza.
“Uganda inazidi kuimarika katika suala la kuikubali dini ya Kiothodoksi. Kumekuwa na mawasiliano mazuri sana kati ya Patriarka Kirill wa Mosko na Urusi yote na Rais Yoweri Museveni. Mimi binafsi niliwasilisha barua kutoka kwa Patriarka Mtakatifu kwa Rais wa Uganda, na tulifanya naye mazungumzo mazuri ya kujengana,” Askofu aliendelea.
“Nchini Uganda, maeneo makubwa yametengwa – hekta 6.5 – kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kiroho na kiutawala cha Kanisa la Kiothodoksi la Urusi. Pia, kwa makubaliano na Rais Museveni, tutajenga jengo la shule ya awali ya watoto, shule ya elimu-jumuishi, hospitali na majengo mengine kadhaa kwa ajili ya huduma za kijamii na kibinadamu, “Askofu Mkuu alisema.
“Tuna matarajio mazuri sana nchini Uganda, na kama Bwana atasimamia kila kitu, basi nadhani Uganda itakuwa “kitovu cha kiroho” cha Kanisa la Kiothodoksi la Urusi katika Afrika Mashariki,” kiongozi huyo alisema.
“Tunakwenda kwa kasi nzuri sana: ndani ya mwaka mmoja tu tumeweza kuingia katika nchi 18 za Afrika. Ninakiri, kama mkuu wa Esarkia, nilikuwa nikitegemea kuingia kwa polepole zaidi,” alihitimisha Metropolitani wa Klin Leonid. Watu wengi wanajiunga nasi, wengine wakitokea mahali ambako hapajawahi hata kuwa na makanisa. Na endapo hali hii itaendelea hivi, basi katika miaka mitatu hadi mitano ijayo tutaweza kuenea karibu katika bara zima la Afrika na kuhakikisha uwepo kamili wa Kanisa la Kiothodoksi la Urusi,” Metropolitani wa Klin Leonid alihitimisha.