Askofu Mkuu Konstantine, Patriarko Eksarka wa Afrika, amepewa jina la cheo cha Jimbo la Cairo na Kaskazini mwa Afrika" - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT

Askofu Mkuu Konstantine, Patriarko Eksarka wa Afrika, amepewa jina la cheo cha Jimbo la Cairo na Kaskazini mwa Afrika”

Mnamo Julai 24, 2025, kufuatia mkutano mkuu wa Sinodi Takatifu ya Kanisa la Orthodox la Urusi uliofanyika Moscow.

Washiriki wa Sinodi hiyo walikuwa na maoni juu ya vyeo vya maaskofu wa Majimbo ya Upatriarka wa Eksarketi ya Afrika (Jarida No. 84).

Sinodi iliamua kwamba askofu anayeongoza Jimbo la Afrika ya Kaskazini, anapaswa kuwa na cheo hicho cha ” Jimbo la Cairo na Kaskazini mwa Afrika.” Pia Askofu mkuu wa Afrika ya Kusini amepewa jina la cheo cha Jimbo la “Johannesburg na Kusini mwa Afrika”.

Hivyo Sinodi imeamua kumteua Askofu mkuu Konstantine wa Zaraisk, Patriako wa Eksarka wa Afrika kuwa Askofu Mkuu wa Cairo na Kaskazini mwa Afrika, ambapo makao makuu ya Jimbo hilo yatakuwa Cairo. Na atahudumu Jimbo la Johannesburg Afrika ya Kusini kwa muda mpaka atakapoteuliwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo.

Shirikisha katika mitandao ya kijamii: