Dayosisi ya Afrika ya Kaskazini iliundwa kwa azimio la Sinodi Takatifu la tarehe 29 Desemba 2021 (Jarida Na. 100), ikiwa ni sehemu ya Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika.
Eneo la uwajibikaji kihuduma za kichungaji ni: Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Jamhuri ya Sudani, Jamhuri ya Sudani ya Kusini, Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Dola la Eritrea, Jamhuri ya Jibuti, Jamhuri ya Shirikisho la Somalia, Jamhuri ya Shelisheli, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kameruni, Jamhuri ya Chadi, Jamhuri ya Shirikisho la Nigeria, Jamhuri ya Niger, Dola ya Libiya, Jamhuri ya Tunisia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, Ufalme wa Moroko, Jamhuri ya Kabo Verde, Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania, Jamhuri ya Senegali, Jamhuri ya Gambia, Jamhuri ya Mali, Burkina Faso, Jamhuri ya Guinea-Bisau, Jamhuri ya Guinea, Jamhuri ya Sierra Leone, Jamhuri ya Liberia, Jamhuri ya Kodivaa, Jamhuri ya Ghana, Jamhuri ya Togo, Jamhuri ya Benin.
Katika muundo wa Dayosisi hiyo pia zilijumuishwa parokia za Stavropol, za Patriarkia ya Mosko, zilizoko katika Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Jamhuri ya Tunisia na Ufalme wa Moroko.
Cheo cha Askofu Kiongozi: " Wa Kairo na Afrika ya Kaskazini".
Askofu mtawala: Askofu mkuu Konstantin wa Zaraisk.